Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 5,628
- 6,411
Hakuna mtu atakayekuja kukuambia au kukufundisha ukweli. Ukweli unafahamika na unapatikana kupitia kufahamu. Kufahamu ukweli ndiyo ukweli wenyewe na hiyo ndiyo maana ya maana ya kufahamu kweli.
Jamii ina namna yake inayotaka mambo yafahamike ndiyo maana ipo mifumo mingi sana leo Duniani ambayo kwa kiasi kubwa inawataka watu kuelewa mambo kwa namna ileile iliyopangwa.
Leo wanaofahamu ukweli wanaonekana kama ni waasi fulani hivi kwa sababu Jamii inawaona kama hawapiti katika njia ileile. Ukifanya utafiti utagundua hata viongozi wengi waliokuwa chachu ya mabadiliko makubwa ya kijamii na kisiasa katika Jamii zao walionekana kama waasi kwa sababu hawakupita njia ileile.
Ukweli ndiyo uhuru halisi wa binadamu, uhuru ambao kuupata Kuna gharama za kutengwa, kuonekana msaliti, kuoneka muasi au kuwa kinyume na wengi. Uhuru huu ndiyo uhuru mgumu kuupata Duniani kuliko kitu chochote kile.
Kuiishi kweli baada ya kuifahamu ni maisha mengine magumu sana kutokana na mifumo ya kijamii iliyojikita katika nyanja zote za maisha.
Maisha ya mtu anayeifahamu kweli katika mifumo iliyopo ni maisha ambayo Jamii pana ikiyaona hauwezi kuyatanani licha ya ukweli kuwa maisha hayo huwa chaguo sahihi kwa aliyeifahamu kweli.
Maisha ya kuishi nje ya mfumo ni maisha fulani ya kipekee sana, maisha ya kuwaonea huruma wengi ambao kwa hakika hata wao wenyewe hawajionei huruma.
Kwa muda nimejaribu kufuatilia maisha ya watu walioweza kuinua ufahamu wao kiwango cha kuitazama mifumo Jamii chini yao yajiwa yamejawa upweke na kutengwa lakini cha ajabu watu hawa huwa na furaha siku zote hata katika mazingira ambayo wengi tunaona kuwa hawapaswi kufurahi.
Ukweli humuweka mtu huru kiasi cha kutoyaona maumivu yoyote ambayo watu waliopo ndani ya mfumo huyaona. Tumeshuhudia furaha na tabasamu katikati ya mazingira magumu ambayo tunatazamia kila mmoja kuhuzunika.
Tumeona tabasamu zuri kwenye nyuso za baadhi wapendwa wetu waliotangulia licha ya ukweli kuwa kifo kinaumiza. Malezi zaidi ya upande wa pili tunaweza tukayakosa ila mtu anapofahamu huwa huru.
Haipo njia rahisi ya kuwa huru bila kuifahamu kweli. Kweli imefichwa sana na inapotoshwa kila uchao. Taasisi zote kubwa za kijamii zinatuandaa kuishi katika namna ileile iliyopangwa na watu na siyo iliyopangwa na asili.
Jambo ambalo sina shaka nalo ni hakika kuwa ukweli tunaufahamu ukiwa ndani yetu. Tumeumbiwa ukweli "we are wired with truth". Tunazimwa kila siku kuukumbuka ukweli huo licha ya kuwa na mashaka mengi juu ya mambo mengi ambayo tumekuwa tukiambiwa ni kweli.
Safari ya uhuru wa kweli imefungamana sana na kuifahamu kweli. Ni safari ya kila mmoja wetu katika Dunia hii. Tumeumbwa ili kuifahamu na kuifahamu ndiyo kufahamu kweli. Safari hii imekuwa ikizimwa katika kila hatua ya maisha ya mtu, tangu kuzaliwa mpaka kufa.
Kufahamu ukweli ni sawa na mfano wa kufa "wanaolia na kuhuzunika ni waliobaki"