Mtaje Golikipa wako pendwa zaidi katika soka

Hili la hakuwahi kufungwa umetupanga, hakuna kipa ambaye hakuwahi kufungwa.
Kama unamjua tuambie hapa ni nani aliyemfunga Masajjage. Hata Joe Kadenge mwenyewe aliwahi kukiri kuwa Masajjage alishindikana; inawezekana pia humjui Kadenge
 


Nafikiri hujui kiingereza, hivyo hukuelewa yaliyoandikwa kwenye gazeti hilo ulilokwoti.

Nitakusaidia kulielewa. Kwanza kabisa tambua kuwa timu ya Simba iliyoandikwa humo siyo hii ya Msimbazi.

Mwaka 1977 wakati wa utawala wa Amin, timu ya Express FC ambayo kapteni wake alikuwa Masajjage ilicheza na timu ya Simba FC ambayo ilikuwa ni ya jeshi la Uganda ikitokea Simba Batallion. Katika mchezo huo Express iliifunga Simba ambao 2-0. Wanajeshi baada ya kufungwa wakaitembezea Express mkong'oto wa nguvu sana kwa hasira za kufungwa. Masajjage hakufungwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…