Mtaje mchezaji ambaye hujawahi kumuona akicheza ili wakongwe wakuchambulie sifa zake

Mtaje mchezaji ambaye hujawahi kumuona akicheza ili wakongwe wakuchambulie sifa zake

Huu ni uzi maalum wa kutaja wachezaji wa zamani ambao hukuwahi kuwaona wakicheza. Ukishawataja subiria wakongwe waliomuona akicheza waje wakuoe sifa zake.

Mimi sijawahi kumuona George Magere Masatu akicheza, naombeni mnitajie uwezo wake maana yupi hyped sana
Ukiacha ufupi wake kuna wakati aliokoa mipira ya kichwa iliyokuwa inaenda golini.Alisifika kwa uwezo wa kuokoa mipira ile ambayo ilikuwa ikielekea golini kabisa.Huu ulikuwa ni mmoja wa upekee wake.Alichezea pamba ya mwanza mengine wataongeza wadau.
 
Wote nimewaona,maclip yamejaa youtube huko
Niletee Clips za Hussein Amani Masha; George Magere Masatu, Beki Mstaarabu Samli Ayoub, Deo Njohore OCD, Golden Boy Zamoyoni Mogella; Said Mwamba Kizota, Ball Juggler Malota Somo.... , Ahmed Amasha.... na Kwa majirani zetu beki mwenye akili kutoka Zambia Marehemu Eston Mulenga.....
 
Hahaha huyu bwana namsikia sana nikiwa mdogo.

Edibile Lunyamila..sijui kama nimepatia jina.

Wakubwa wetu, sifa zake.
 
Sijawahi kuwaona wakicheza 'Edibily Lunyamila na Mohamed Husein & Rashid Mandanje -Wote hao nasikia waliwahi kucheza Yanga
 
Back
Top Bottom