Uko sahihi kabisa Mkuu, tena kipindi hicho Balhabou alikuwa mmoja wa Wafadhili Wakubwa wa Klabu ya Simba. Alimpa kimemo Haruna Moshi kwa ajili ya kuwapa viongozi wa Simba ili waweze kumsajili. Alipowapelekea kimemo hicho Viongozi wa Simba, alipelekwa moja kwa moja uwanjani kwa ajili ya kufanyiwa majaribio. Haruna Moshi "Boban" aliupiga mpira mwingi sana siku hiyo. Hata hivyo, kutokana na ukiritimba wa viongozi wa Soka wa Klabu ya Simba wa wakati huo alielezwa kuwa aongeze kiwango kwa kuanzia Timu B ya Simba ndio wamsajili. Haruna alirudi Morogoro na kumwarifu yote yaliyotokea kwenye majaribio yake Bwana Balhabou. Balhabou aliwapigia simu Viongozi wa Simba na kuwaambia kuwa kama hawatamsajili Haruna Moshi basi huo ndio utakuwa mwisho wa ufadhili wake kwenye Klabu ya Simba. Hivyo, Viongozi wa Simba wakakubali kwa shingo upande kumsajili Haruna kutokana na shinikizo la Balhabou. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa Haruna Moshi kuchezea Klabu ya Simba.