Mtaji milioni 3, biashara ipi itafaa?

Mshana kakupa wazo zuri sana, ni wazo ambalo unaweza kusimamia vizuri kwa sababu wewe ndio mwenye kuhesabu pair za viatu, na kupanga bei kwa aina za viatu, kisha mtu ambae atauza atatekeleza kile ulicho kipanga wewe.

Cha msingi utumie daftali na karamu kwa kila kitu.
 
Mkuu tufanye hiyo kazi.

Nipe, Mtaji unaanzia kiasi gani...kifupi nipe mchanganuo.

Ila masharti ni vema nikapafahamu kwako.

2. Nikawajua wazazi wako/walezi na tukaandikishiana Mkataba kisheria...ambao una terms and condition halafu tunakuwa Maarafiki wazuri sana kwenye hiyo Biashara kwasababu Uaminifu utakuwa juu sana...
 
Huwezi eleza kwa mtu mwingine mka/tuka gawana hiyo%?
Hii biashara nimeshawaekezea watu zaidi 3 humu lakini watu wamezoea biashara za kisharobalo ni ngeni kwao wakati wachina wanakamata frusa
 
Bintishomvi mie nipo Dar leta huo mchanganuo tutoke wote.
Ni biashara ya plastic chakavu naielezea kila siku watu wamezoea biashara za mazoea hii ni biashara mpya kwao China ni ya Zamani wanakuja wananunua wanaenda wekeza kwao napata hasira sana pesa imeniangusha
 
Fuga Sungura kupitia shirika letu! Kwa fedha hiyo sisi tutakujenge banda! Tutakuletea Sungura 12 ,chakula madawa na ushauri!! Mwisho sisi tutanunua Sungura wote watakaozaliwa wakiwa na miezi 4 tu!

Wastani wa sh 32,000 hadi 40,000 kwa Sungura! Sungura mmoja anazaa watoto 6 hadi 15 Sungura anazaa kila mwezi, hivyo kwa mwaka atazaa Mara sita kwa kuwa atanyonyesha mwezi mmoja!! 6*6*10 = 360
360*32,000 =??????? Je fedha yako haijarudi? Tuwasiliane 0715829576
 
Mbona umeweka kirahisi hivyo, kwamba Mtu akupe tu wazo la maana la biashara kama vile mmekutana tu njiani?.

Mawazo mengine huenda ni Mtu alipanga kufanya jambo ila labda mtaji akakosa, sasa unatarajia akupatie wewe hilo wazo kirahisi tu?. sio kwamba na wewe usema naye atanufaika vipi, yaani "win win situation".

Hayo ni maoni yangu tu.
 
Ngoja nikusaidie chap!
Nenda kahama kule machimbo kwa wale wachimbaji wadogo wadogo uwe unafanya kuwasupply na huduma za oxygen. Pia ukiona hio haifai basi anza kubroker madini kwa hao hao wachimbaji wadogo. Ukiona hio ni risky sana basi ingia

Plan B
Vizia msimu wa mavuno haswa kwa mazao ya iliki, pilipili manga na vanilla kusanya mzigo wa kutosha huko mashambani kisha weka stock ndani. Subiri mwezi wa 3 ambapo soko huwa zuri sana uuze.

Plan C
Anza kutengeneza spirits vinywaji kwa mtindo wa gongo ila uwe na tbs.

Plan D
Nenda huko vijijini kutana na waganga na wataalam wa tiba za kiasili wakufundishe dawa mbalimbali, kisha rudi mjini anzisha duka lako la dawa za mitishamba na nguvu za kiume.

Plan E
Nunua mahindi ya kutosha safirisha kule Congo ukifika unatoa mzigo bure unapewa madini bure.

Plan F
Tafuta waremboo wa vyuoni kisha uwe unawaconnect na wadau wenye uhitaji.
Itaendelea.........
 
Ngoja nikusaidie chap!
Nenda kahama kule machimbo kwa wale wachimbaji wadogo wadogo uwe unafanya kuwasupply na huduma za oxygen. Pia ukiona hio haifai basi anza kubroker madini kwa hao hao wachimbaji wadogo...
Duuh..kwahiyo jamaa awe na danguro?

#MaendeleoHayanaChama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…