Mtaji ninao tatizo muda, nifanye biashara gani?

Mtaji ninao tatizo muda, nifanye biashara gani?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Hii mada nairudia tena kwa mara nyingine, mtaji ninao wa zaidi ya million saba tatizo kazini natoka Kuanzia saa 9 na nusu usafiri ninao pikipiki. Job kila siku Monday to Friday na pia ni mtu wa site mara kwa mara haipiti mwezi lazima kuna siku tano mpaka 10 niwe safari.

Je biashara gani ambayo bidhaa zake haziharibiki na vile vile ukiwa haupo haithariki yaani hupotezi wateja kila siku wateja wapya wanapita..

NB: Sitaki kumuweka mtu nataka iwe ya kuisimamia mimi...nilikuwa nawaza labda niwe na kibanda cha asali barabarani niongezee na idea nyingine nzuri.
 
Hii maada nairudia tena kwa mara nyingine.mtaji ninao wa zaidi ya million saba tatizo kazini natoka Kuanzia saa 9 na nusu usafiri ninao pikipiki.job kila siku Monday to Friday na pia ni mtu wa site mara kwa mara haipiti mwezi lazima kuna siku tano mpaka 10 niwe safari...je biashara gani ambayo bidhaa zake haziharibiki na vile vile ukiwa haupo haithariki yaani hupotezi wateja kila siku wateja wapya wanapita..

NB:sitaki kumuweka mtu nataka iwe ya kuisimamia mimi...nilikuwa nawaza labda niwe na kibanda cha asali barabarani niongezee na idea nyingine nzuri.
Hakuna biashara utafanikiwa peke yako
Keki ni kubwa saana
Wekeza kwa watu
 
we ni mpare?
em ajir mtu
Biashara gani na ukiwa mbali Jamaa awe mwaminifu...na kumbuka nipo mkoa wa ugenini mwaka wa pili sasa na vijana sio waaminifu Nadhani unaelewa mikoa ya pwani ya kusini vijana sio watu wa kazi
 
Nimeshawekeza kwa watu biashara ya nguo nilichofanyiwa sio poa..ndo maana hata imani kwa watu imepungua ndugu
Kaka maisha ndio yalivyo makosa yapo ili kutufunza kuna namna ya kusimimamia biashara yako huenda ulifeli hapo je umejifunza ?

Pili unaweza usiwe unamiliki biashara hiyo ila ukawekeza kupata faida kutokana na hisa zako

Tafuta watu makini wa kufanya nao kazi
Biashara inataka usimamimizi imara sio rahisi kama unavyotaka iwe
 
Nunua pikipik mbili au Tatu wape vijana mkataba wanakuwekea Kila baada ya siku 5 au Saba iyo haiathir chochote ila tafuta vijana waaminifu na mkataba uwe wa kimaandishi
 
Achana na biashara, iyo pesa kanunue kiwanja ambacho kitapanda thamani mpaka pale utakapopata akili ya kufanya shughuli maana nacho kiwanja kitakuwa bei juu, au Tunza hiyo pesa bank ama mahala ambako itakuwa safe mpaka pale utakapojiona una muda ama uhitaji wa kufanya jambo la maendeleo, kwa sasa bado hauko na hii akili utaharibu pesa bure.

Ushauri wa bure huu, kazana kutafuta pesa huko unakofanya kazi uku ukiitunza hii pesa na usiiwazie kwa lolote, after 2/more years na uhakika akili yako itakuwa imeshachangamka na hiyo pesa bado iko salama sasa hapo ndipo uamue cha kufanya(hakikisha ulipoitunza imeongeza chochote kitu ndiomaana nmeshauri kuitunza ktk ardhi inayopanda thamani ama mabenki/makampuni yanayotoa huduma za uwekezaji wa pesa kwa kutoa gawio).

Utakuja kunishukuru humu
 
Fungua tena duka la nguo, Ajiri mtu, apige kazi, wewe uwe unapita puta, mishe zako siri yako.
 
Bila raslimali watu huwezi kufanikiwa na huwezi fanya biashara ya goods and services pekee yako.

La sivyo wew una ubinafsi maana sio lazima uajiri mtu wa hapo pwani.

Kwanza kifikira wewe hapo sio mfanyabiashara, huna trust, imagine 7mil. Inaajiri one person, ila hutaki.
 
Hii mada nairudia tena kwa mara nyingine, mtaji ninao wa zaidi ya million saba tatizo kazini natoka Kuanzia saa 9 na nusu usafiri ninao pikipiki. Job kila siku Monday to Friday na pia ni mtu wa site mara kwa mara haipiti mwezi lazima kuna siku tano mpaka 10 niwe safari.

Je biashara gani ambayo bidhaa zake haziharibiki na vile vile ukiwa haupo haithariki yaani hupotezi wateja kila siku wateja wapya wanapita..

NB: Sitaki kumuweka mtu nataka iwe ya kuisimamia mimi...nilikuwa nawaza labda niwe na kibanda cha asali barabarani niongezee na idea nyingine nzuri.
Hela umepata wapi?
 
Kama upo mkoa kama dodoma au dar jaribu na kuaza kuuza simu za smart mfano gogle pixel,I phone n.k uwe unaenda nazo kazini kwenye begi zeni mtafute boda boda muaminifu atakayekua anakufanyia delivery Kwa wateja wako kuhusu kujitangaza tengeneza account za kulipia matangazo Cha msingi jitaidi uweze kujua mlolongo mzima wa simu na wapi wanagumbulia wauzaji wezako Yani kiufupi tengeneza bond na wauzaji wa simu ili iwe rahisi kwako kuaza biashara kwenye simu pesa ipo kama unaweza kutoka malipo njoo nikupambanishie na watu au nikutengeneze option uchague mwenyewe ipi upitanayo
 
Nunua pikipik mbili au Tatu wape vijana mkataba wanakuwekea Kila baada ya siku 5 au Saba iyo haiathir chochote ila tafuta vijana waaminifu na mkataba uwe wa kimaandishi
Hao vijana sasa ndio shughuli ilipo. Ebu nitafutie nikupe boda tatu uwe unaniletea hela besty
 
kwa uzoefu wangu nimechanganua utakalo...unaweza tu kuwekeza kwenye capital gain but its not business....ina risk ndogo na profit huwa ni ndogo na inahitaji fedha nyingi wakati mwengine ili iweze kukimu matumizi yako...capital gain ni aina ya shughuli wengine huiita biashara ya kuweka stock..ila kiuhalisia sio biashara...biashara ni kununua na kuuza au kutoa huduma hii unanunua unahold kwa kipindi fulani then unauza bei ikichangamka..kuna la kujifunza pia kama unataka kufanya hii shughuli...store ya bei nafuu na salama kwa wezi wadudu au wanyama ..uzuri ushakuwa na wazo la asali..nunua asali kwa usafi unaohitajika(msisitizo) unaweza kununua taka ukajua ni asali kama huijui asali achana nayo hio shughuli au jifunze abc za asali..wakati wa mavuno huwa bei nafuu na kuna kipindi inapanda bei..sikonge na tabora nimefanya mara kadhaa na wateja ni wakenya africare na mchina yupo dsm sijui huko ulipo kama utapata wateja...au nunua mazao kama mpunga hayana ykorofi wa kuhold stock,mahindi ni mtiti, kuhifadhi ila ukiamua unapambana nayo...biashara inataka muda hasa wa kusoma customer physiology na movement yao..vinginevyo utalaumu vijana mara wasidizi.....au fanya kama rafiki yangu mwalimu nilimkuta vijijini huko nzega mwamala ana duka la pepsi jumla jioni ikifika anachoma mishikaki na kuuza juice na chips...naye anafanya na msaidizi mmoja duka lajumla vinywaji ni rahisi kuuza ila faida kiduchu sana kwa kreti yapata 500 hadi 1500.
 
Back
Top Bottom