Mtaji si kigezo cha kuanza biashara bali bongo lako - jadili

Mtaji si kigezo cha kuanza biashara bali bongo lako - jadili

Ni kweli kabisa, Ila ishu ni kwamba si kweli kabia kwamba unaweza kuruni biashara bila mtaji kwa sababu hata servise business ambzo inasemekana unaweza anza bila mtaji still lazima uwe na hata Tsh 500 ya kununua kalamu au karatasi na kazalika,

So ishu ni kwamba Kama Mjasiriamali unatakiwa kuumiza kichwa jinsi ya ku grow, huwezi ukajiita Mjasirimali halafu ukaanza kulia kwamba huna mtaji,The real Entreprener hasubirii mapka serikali ilete miradi ya Ujasirimali ndo aanze,

Ni kweli Iadea ni Primary capital na kutokea hapo ndo unaweza wewe kama wewe kuumiza kichwa jinsi ya kuweza kusonga mbele na wazo lako, watu wasiishie kusema wana mawazo ya Biashara ni lazima Uonyeshe bidii katika wazo, Wazo kama wazo si ishu kabisa na watu hawawezi kukuona mjanja kisa un wazo bali utapimwa kwa jitihada zako,

Hivyo Basi, swala la Mitaji ni juhudu za Mtu bianafisi, nazani ukisoma story za watu wali fanikiwa, kuna story zinazungumzia walivyo grow up, so ni wewe kama mjasiriamali kuhangaika kwa kila njia ya kupata pesa za kuanza projet yako

Kwa Bongo Tunatatizo kubwa sana katika hilo, Mtaji umegeuzwa kuwa Ngao ya Kuharalisha mtu kuto kujiajiri, kila utakaye muuliza ni mtaji,

Ukiwa na Spirit ya Ujasiriamali utaona kwamba mtaji si ishu kabisa, Bali kinacho takiwa ni Jitihada binafisi, unaweza kuta mtu ni mfanya kazi naanalipwa freshi tu ila swala la Kujiajiri atakuambia hana pesa, ishu ambayo sio kweli,

SO KWA WAFANYA BIASHARA MTAJI KWELI NI TATIZO KUBWA SANA, ILA KWA MJASIRIAMALI MTAJI SI TATIZO,

Sifikirii kwamba lazima mtu uwe na mtaji wa pekee, ninachofikiria akili, utashi na nguvu zetu ni mtaji tosha. Fikiria ukiamua kwenda porini kuokota mzigo wa kuni na kisha kumwuzia anayezihitaji sidhani kama kuna mtaji wa pekee isipokuwa nguvu zako na matumizi yako ya kawaida nyumbani ambayo wayatumia kila siku.

Kama leo umefanikiwa kuuza mzigo wa kuni kwa fulani umeingiza cho chote mfukoni na kisha mnunuzi atawajuza majirani nao watataka kuni, hapo umeshapanua wiko wa soko licha ya mwenyewe kutafuta wateja zaidi. Mtu wa aina hiyo unafikiri hajaanza mtaji na kisha kuamua kutunza mapato yake, sitashangaa siku akifanikiwa kununua mifuko miwili ya sement na kifyatulio cha blocks na kuanza mtaji huo kiwanda cha kufyatua block za kujengea zinazohitajika kila siku. Huhitaji kuhangaika kutafuta maji ya gharama, anzisha mradi kando ya kijito wenye nazo watakufuata tu.
 
mi naona huwa tunahamasishana tu. bila mtaji haiwezekani jamani, unaanzia wapi kwanza????
 
Mkuu Candid Scope, Heshima yako.

Kuna kitabu hapa katika pdf nakiambatanisha ili kukazia mada yako, kinaitwa ''The Science of Geting Rich''. Chukueni jamani mkisome, kama kuna mwingine anahitaji vitabu vingine kama hivi aniambie nitatoa kadri ninavyopata muda.
 

Attachments

Mkuu Candid Scope, Heshima yako.

Kuna kitabu hapa katika pdf nakiambatanisha ili kukazia mada yako, kinaitwa ''The Science of Geting Rich''. Chukueni jamani mkisome, kama kuna mwingine anahitaji vitabu vingine kama hivi aniambie nitatoa kadri ninavyopata muda.

Nimekisoma na nimekipenda, very interesting!
 
Back
Top Bottom