Na kwa kuongezea Mkuu
Kwa hapa Tanzania Kuna Tatizo kubwa sana katika swala zima la Kuhamasisha Ujasirimali, Tofauti na Mataifa Mengine hata ya Africa, Ulaya, na Asia, Nchi kama China kwa sasa Entreprenership iko juu sana kutokana na Mwamko, India ndo kabisa Spriti iko juu mno,
Kwa Tanzania tuna kwaza na vitu vifutavo
1. Mfumo wa Uchumi wetu zamani- UJAMAA
Ujamaa ni mbaya sana katika swala zima la kujenga Entreprenership, na Mataifa kama Urusi kwa sasa wanapata shida sana, na China sema ilishutuka mapema inagwa hata wao wana matatizo na wawekezaji wengi walioko China wametokea JAPAN,KOREA, USA NA ULAYA
'Ujamaa hautoi nafasi kwa ukuwaji wa Ujasirimali na hii ni kutokana na serikali kufnya kila kitu,
2. MAZINGIRA
Vijana wengi mazingira walio kuria haya hamasishi ujasirimali kabisa, Tukiwa watoto Wazazi wetu walikuwa ni Wafanya kazi, Ndugu zetu wengi ni wafanya kazi, Majirani ni wafanya kazi, so tumekuwa tukishuhudia Wazazi wakija kuchukuliwa na Magari ya Ofisi, tukawa na sisi tunatamnai kuwa kama wao
Baba anaenda safari na Gari la Ofisi akirudi anakuja na Mizigo kibao iliyo bebwa kwenye hilo gari kama Mkaa, na kazalika, tukawa tunatamnai, Wazazi wanaleta baadhi ya Vitu vya kazini kwao tukawa na sisi tunatamnai sana
Majinari wote ni wafanya kazi na tunatamani kuwa kama wao
Ndugu wote ni wafanya kazi na tunatamani kuwa kama wao
Cheki watoto wa Kihindi- baba mfanya baisahara, Mama mfanya biashara, Majirani wafanya biashara, Marafiki wafanya biashara, wajomba wafanya biashara, hapa usitegemee watoto waje kuwa wafanya kazi NEVER
3. MAKUZI KUTOKA KWA WAZAZI
Haya yanachangia asilimia zaidi ya 50 katika kuondoa hari ya Ujasirimali nchini, Tumekuwa tukikuzwa na kuambiwa inatakiwa tusome tuje kuwa Mameneja, Wakurugenzi, tufanya kazi Benki na kazalika, hii inajengeka kichwani mwa Mtoto anaenda Shule akiamini anatakiwa asome aje kuwa Meneja
KWA STAILI HII NI LAZIMA KIJANA AWE NA HARI YA KUTAFUTA KAZI NA SIO KUJIAJIRI
5. MASHULENI
Hapa ni kama wazazi, nako walimu story ni za kiajiriwa tu na hata wano tufundisha wameajiriwa so ni kwa nini sisi tujiajiri
6. MFUMO WA ELIMU
Ingawa si kwa sana, but hata mfumo wa elimu yetu unatufanya tuogope biashara sana, Elimu ya Kukaririshana, Elimu ya Kusoma Handout, Elimu ya kusomea siku ya paper, Elimu ya Kusoma Mapast paper mwanzo mwisho,
Hizi aina za kusoma kwa kweli zinaondoa udadisi, zinatufanya tuwe tegemezi zaidi na zaidi
7. SERIKALI YETU KUKOSA UHAMASISHAJI
Nchi nyingi Duniani zaina vitu vya kuvutia Vijana kuwa wajasirimali ikiwemo Mikopo au Grants za kuanzishia biashara, na Nchi kama India vyuo vikuu vyao vingi vijana wanao jiajiri ni wengi kuliko wanao enda mtaani kutafuta kazi, sasa njoo Bongo nenda hata SUA uone 99% ya wanachuo wanataka waajiriwe
8. MFUMO WA WATANZANIA
Nchi kama Kenya au Nigeria na kwingineko hari ya Kujiajiri iko juu sana kutokana na Mfumo wa Maisha yao, Nchi kama Kenya Maisha ni Magumu sana na hakuna Ndugu wa kukusaidia, hakuna Pesa ya Bure, hakuna cha Shangazi, Mjomba, shemeji wala nini, kwa staili hii kijana ni lazima akomae make no way out,
Nchi kama Nigeria maisha ni magumu sana na ndo maana vijana wanakuwa hadi matapeli wa kimataifa ni kutokana na kwamba hakuna wa kumsaidia,
TANZANIA, Huku maisha ni rahisi sana, mtu ukiona hakieleweki unaibuka Kwa shemeji unaishi hata miaka mitano kule na unakula na kulala bure, ni kwa nini uhangaike wakatiu unakula na kulala Bure? Ukiwa nyumbani kwenu ndo kabisa unaweza Oa na ukaleta mke nyumbani kwenu na Baba na Mama wakawa wanawahudumia bila tatizo kabisa, so ni kwa nini uhangaike wakati kwenu hujafukuzwa?
Ukiona vipi unajichanganya kwa Baba mdogo, Shangazi, Mjomba, Kaka, Binamu, Bibi, Babu, kwa BABA WA UBATIZO na kazalika,
Kwa wenzetu hakuna kitu kama hicho hapo Kenya hakuna mambo kama haya, so kijana ni lazima hata akimaliza Chuo kikuu awe mpiga DEBE make hana njia nyingine ya kushi, hakuna wa kumsaidi
SO HAYA MAMBO YA KUENDEKEZANA YANALEMAZA SANA TENA MNO, NA YANAFANYA VIJNA WAWE DEPENDANT