Mtaji siyo tatizo kwa walio wengi, tatizo ni sisi wenyewe kutojua jinsi ya kuanza.

Mr. Aweda hii ni shule kubwa na nzuri kabisa.. Umeieleza katika lugha rahisi kabisa.. Mimi nilikuwa mbishi sana na muoga wa kuanzia chini, Kisa nilihudhuria tu darasani na kupata vyeti visivyosaidia kwa mtu kujiajiri.. Nilifanya kazi, tena katika nafasi nzuri kwa miaka saba ila sikuweza kujikwamua kiuchumi zaidi ya kuwa na madeni makubwa ya magari na nyumba ambayo sikuweza kuimaliza.. Nilifanikiwa kwenda kusoma nje kwa miaka 4.. Nilikutana na watu wengi toka west africa wenye spirit ya ujasiriamali.. Niliporudi Tz sikutaka kabisa kurudi kwenye ufungwa wa kazi.. Kwa mtaji mdogo sana nilioanza nao sasa ni karibia mwaka mmoja nauona mwanga na nimeshajikomboa kwenye MTEGO WA MSHAHARA.. Mimi ndio nimewaingiza vijana sasa wanitumikie..
 

Safi sana mkuu,
 

thank you
 

Kila kitu ni lazima tupinge! Usijali, ndio zetu JF.
 

Thank you. Umeeleweka vizuru sana.
 
Na kwa kuongezea Mkuu

Kwa hapa Tanzania Kuna Tatizo kubwa sana katika swala zima la Kuhamasisha Ujasirimali, Tofauti na Mataifa Mengine hata ya Africa, Ulaya, na Asia, Nchi kama China kwa sasa Entreprenership iko juu sana kutokana na Mwamko, India ndo kabisa Spriti iko juu mno,

Kwa Tanzania tuna kwaza na vitu vifutavo

1. Mfumo wa Uchumi wetu zamani- UJAMAA
Ujamaa ni mbaya sana katika swala zima la kujenga Entreprenership, na Mataifa kama Urusi kwa sasa wanapata shida sana, na China sema ilishutuka mapema inagwa hata wao wana matatizo na wawekezaji wengi walioko China wametokea JAPAN,KOREA, USA NA ULAYA
'Ujamaa hautoi nafasi kwa ukuwaji wa Ujasirimali na hii ni kutokana na serikali kufnya kila kitu,

2. MAZINGIRA
Vijana wengi mazingira walio kuria haya hamasishi ujasirimali kabisa, Tukiwa watoto Wazazi wetu walikuwa ni Wafanya kazi, Ndugu zetu wengi ni wafanya kazi, Majirani ni wafanya kazi, so tumekuwa tukishuhudia Wazazi wakija kuchukuliwa na Magari ya Ofisi, tukawa na sisi tunatamnai kuwa kama wao

Baba anaenda safari na Gari la Ofisi akirudi anakuja na Mizigo kibao iliyo bebwa kwenye hilo gari kama Mkaa, na kazalika, tukawa tunatamnai, Wazazi wanaleta baadhi ya Vitu vya kazini kwao tukawa na sisi tunatamnai sana

Majinari wote ni wafanya kazi na tunatamani kuwa kama wao

Ndugu wote ni wafanya kazi na tunatamani kuwa kama wao

Cheki watoto wa Kihindi- baba mfanya baisahara, Mama mfanya biashara, Majirani wafanya biashara, Marafiki wafanya biashara, wajomba wafanya biashara, hapa usitegemee watoto waje kuwa wafanya kazi NEVER

3. MAKUZI KUTOKA KWA WAZAZI
Haya yanachangia asilimia zaidi ya 50 katika kuondoa hari ya Ujasirimali nchini, Tumekuwa tukikuzwa na kuambiwa inatakiwa tusome tuje kuwa Mameneja, Wakurugenzi, tufanya kazi Benki na kazalika, hii inajengeka kichwani mwa Mtoto anaenda Shule akiamini anatakiwa asome aje kuwa Meneja

KWA STAILI HII NI LAZIMA KIJANA AWE NA HARI YA KUTAFUTA KAZI NA SIO KUJIAJIRI

5. MASHULENI
Hapa ni kama wazazi, nako walimu story ni za kiajiriwa tu na hata wano tufundisha wameajiriwa so ni kwa nini sisi tujiajiri

6. MFUMO WA ELIMU
Ingawa si kwa sana, but hata mfumo wa elimu yetu unatufanya tuogope biashara sana, Elimu ya Kukaririshana, Elimu ya Kusoma Handout, Elimu ya kusomea siku ya paper, Elimu ya Kusoma Mapast paper mwanzo mwisho,

Hizi aina za kusoma kwa kweli zinaondoa udadisi, zinatufanya tuwe tegemezi zaidi na zaidi


7. SERIKALI YETU KUKOSA UHAMASISHAJI
Nchi nyingi Duniani zaina vitu vya kuvutia Vijana kuwa wajasirimali ikiwemo Mikopo au Grants za kuanzishia biashara, na Nchi kama India vyuo vikuu vyao vingi vijana wanao jiajiri ni wengi kuliko wanao enda mtaani kutafuta kazi, sasa njoo Bongo nenda hata SUA uone 99% ya wanachuo wanataka waajiriwe


8. MFUMO WA WATANZANIA
Nchi kama Kenya au Nigeria na kwingineko hari ya Kujiajiri iko juu sana kutokana na Mfumo wa Maisha yao, Nchi kama Kenya Maisha ni Magumu sana na hakuna Ndugu wa kukusaidia, hakuna Pesa ya Bure, hakuna cha Shangazi, Mjomba, shemeji wala nini, kwa staili hii kijana ni lazima akomae make no way out,

Nchi kama Nigeria maisha ni magumu sana na ndo maana vijana wanakuwa hadi matapeli wa kimataifa ni kutokana na kwamba hakuna wa kumsaidia,

TANZANIA, Huku maisha ni rahisi sana, mtu ukiona hakieleweki unaibuka Kwa shemeji unaishi hata miaka mitano kule na unakula na kulala bure, ni kwa nini uhangaike wakatiu unakula na kulala Bure? Ukiwa nyumbani kwenu ndo kabisa unaweza Oa na ukaleta mke nyumbani kwenu na Baba na Mama wakawa wanawahudumia bila tatizo kabisa, so ni kwa nini uhangaike wakati kwenu hujafukuzwa?

Ukiona vipi unajichanganya kwa Baba mdogo, Shangazi, Mjomba, Kaka, Binamu, Bibi, Babu, kwa BABA WA UBATIZO na kazalika,

Kwa wenzetu hakuna kitu kama hicho hapo Kenya hakuna mambo kama haya, so kijana ni lazima hata akimaliza Chuo kikuu awe mpiga DEBE make hana njia nyingine ya kushi, hakuna wa kumsaidi

SO HAYA MAMBO YA KUENDEKEZANA YANALEMAZA SANA TENA MNO, NA YANAFANYA VIJNA WAWE DEPENDANT
 
Hii ndio elimu kwa njia ya mtandao, sio mpaka cheti ndio ujue umefuzu!
Na hii tabia ya kudai huna mtaji wakati mtaji mkubwa na wa muhimu ni uzoefu wa kile unachotaka kwenda kufanya. Ndio maana mabenki wako rahisi sana kumpa mtu mkopo kwa mara ya pili na ya tatu kwani rekodi yake inamlinda, na rekodi ni nini? Ni ule uzoefu wako usiotiliwa mashaka. Tujizoeze kwanza wadau.
 
mkuu nakushauri uanzishe ofisi ya ushauri juu ya masuala ya ujasiriamali. ukianzisha ni-pm nitakuwa mteja wako!
 
mkuu nakushauri uanzishe ofisi ya ushauri juu ya masuala ya ujasiriamali. ukianzisha ni-pm nitakuwa mteja wako!

Consultance business hapa Tanzania Ni ngumu sana, jamaa haijaamka kabisa, mtu akisha ona ana duka na wateja wanakuja kila siku yeye ni basi, Hizi biashara zinalipa sana huko kwa wenzetu, ila sio Tanzania, niliwahi kuifanya huku Arusha kwa kweli ni shida jamii yetu bado sana katika swla zima la Ushauri wa Biashara, wanataka uwashauri bure,
 
ni kweli sisi watanzania hatujajua umuhimu wa kupata ushauri elekezi kuhusu masuala ya biashara na miradi. ndio maana ukifanya utafiti utabaini kuwa watanzania tunabadiri aina ya biashara kila baada ya kipindi kifupi na pia watu wengi wanafunga biashara zao kwa kushindwa kuziendeleza! halafu hapo penye red: ushauri wa bure ni jambo lisilowezekana hata kama ni hapa TZ. siku hizi baadhi ya maeneo hasa DSM imeanza biashara ya kuelekezwa mitaa au ofisi kwa kutoza pesa!
 

Ndo hivyo watanzani wanashindwa kuelewa kwamba hata Makampuni kama VODACOM, TIGO, NA HATA MAKAMPUNI YA MADINI NA HATA YA BIA KAMA TBL pamoja na kwamba ni the reading lakini still wana Consulance firm ambayo kazi yao ni kuwashauri maswala ya masoko, uzalishaji, ushindani na kazalika,

Kwa kifupi Wabongo ni Pasua Kichwa kabisa, Mimi nilisha wahi kukonduct Semina ya kuwapa watu elimu ya Biashara hasa katika Masoko, Ushindani, maswala ya mitaji na kazalika, Cha kusikitisha wale watu waliniuliza kama Kuna Posho, yaani nijitolee and then niwalipe Posho, Tangu siku hiyo niliapa kuto fanya ujinga kama huo kamwe, Ila time is coming amapo watu watakuja kujua hayo mambo,

MWatanzani tunataka tupewe Elimu na Tulipwe, nakumbuka hata NGO Moja ambalo nilikuwa na fanya nalo kazi, tulikuwa tunatoa elimu kwa wakulima huko Bushi sasa ikifika kipindi cha semina, ingawa semina ilikuwa inafanyikia kwenye maeneo yao, wao walikuwa wakiomba Posho na kama hakuna Posho hawaji, Kuna mzungu mmoja ambaye ndo walikuwa wafadhili, baada ya kujionea kwa Macho yake, alimuru muradi ufungwe mara moja na kuapa kuto saidia kamwe,
 
Nakubaliana kabisa na wewe. Kwa kuongezea tu, ningependa kuongelea suala la vijana wengi kushindwa kufanikiwa kwa kuanzia chini kupanda juu. Sababu zifuatazo zinachangia vijana kutaka kuanza biashara kwa milioni 50, 100, 150 n.k kitu ambacho ni ndoto za alinacha:

1. Kwa sasa tunaishi katia ulimwengu wa material world kwa maana ya kwamba, mtu unaheshimika ukiwa na pesa nyingi. Hii inawapa presha sana vijana kufikiria kuanza biashara kwa mitaji mikubwa. Zamani mtu alikuwa anaheshimika kwa busara na mchango wake katika jamii. Hii ilifanya wengi wafanikiwe kwa sababu heshima wanayoihitaji wanayo so wana concentrate kukuza biashara. Siku hizi watu wanaoheshimika ni mapedeshee wanaoimbwa kwenye miziki wakati wazee wenye busara zao wamesahaulika

2. Vijana wengi wa siku hizi hawajiamini na hawana uwezo wa kufikiri kivyao. Vijana wengi siku hizi ni waoga wa kufanya mambo kutokana na woga wa kufikiria watu wengine watawafikiriaje wakiwaona wanafanya biashara ndogondogo. Hii inatokana na malezi tunayopata ambayo hayasaidii kupandisha morali na kujiamini kwa watoto wa kitanzania.

3. Ukosefu wa elimu ya biashara. Watu wengi wanaopenda kupata faida za haraka haraka hawajui kwamba ukiwa na elimu ya biashara itakusaidia kupata yote hayo badala ya kuiba, kwenda kwa waganga wala kuua watu. Ukiwa na elimu ya biashara itakusaidia kujua jinsi gani ya kuvutia wateja na kukuza biashara fasta.

Nasema haya yote kwasababu mimi mzazi wangu ameshawahi kushika nafasi kubwa kiaina serikalini, so mimi tokea mdogo ninaona mashangingi yakimchukua na kumpeleka kzini na pia kuishi kwenye nyumba za kifahari za serikali. So akili yangu ilikuwa ni kuanza biashara kwa milioni 100 ili kuweza kuishi lifestyle kama hiyo. But nilipoenda kusomea bishara ndo nikagundua kwamba hata nikiwa na 500,000 naweza ikuza na ikanipa yote hayo. Ni ishu ya kupata elimu na kuchange mindset kiaina.
 
Uko sahihi sana mkuu, hata mimi mwenyewe najishangaa kwani najiuliza ninaweza kufanya biashara gani, nimekuja kugundua kuwa mtaji ninao ila wazo la biashara ndo sina, japo mtaji si mkubwa (ni mdogo sana lakini ninawafahamu watu wengi ambao wan biashara zenye mtaji mdogo zaid ya mtaji wangu.
Kweli umesema sawa jambo kubwa ni kuwa na elimu ya ujasiriamali.
Ahsante sana ndugu yangu
 
Samahani kwa kutofautiana kidogo,kwa mtazamo nilionao nafikiri kitu kikubwa kabisa kinachotushinda ni ule uthubutu/Nia wa/ya kufanya maamuzi kwa kuogopa changamoto zilizopo.Mawazo yetu labda yanakuwa yanafikiri eti biashara ni kama mchezo wa kamali ya kubahatisha,na wakati mwingine ni kweli kotokana na aina ya biashara husika.

Hivyo basi tuliowengi tunaogopa kuingia katika majanga yaliyo katika biashara,ambayo wakati mwingine ni hatari sana kibiashara na kwa mhusika mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…