Mtaji TZS 1 Million, naombeni ideas za biashara

Joined
Jan 12, 2015
Posts
55
Reaction score
19
Wadau hasa wajasiriamali wazoefu nina mtaji wa 1m madafu naombeni ideas za biashara nijikwamue kiuchumi. Ajira zenyewe ngumu na serikali ikishakufaga kitambo ujanja kujiongeza kivyako
 
tafuta mtu anaefuataga bidhaa china mpe akanunue smart phone kwa bei rahisi then uje uziuze mavyuoni ili mtaji uwe mkubw
 
kuna ushauri hapo wa smartfone ni mzuri kama ukiwa na taarifa nzuri za manunuzi ya huko na ukimpata mtu mwaminifu atakae kulindia hiyo hela yako maana mmmmh! mimi nakushauri watafute jamaa wanao uza pweza uwaombe wakufundishe kuchoma pweza na kutengeneza bagia hakika ukifanikiwa kujua basi utaanza na kuajiri vijana hata8 kwa mil moja yako hiyohiyo, ila sasa hiyo hela usianze kwa kuiona ndogo hutafanikiwa hata kidogo..asante.
 
Kama uko morogoro au dar,nenda morogoro huko kilosa uwe unanunua madini yanaitwa feldspar uwe unakuja kuyauza dar.

Unanunulia kilo moja 2000 au 2500,dar yanatoka kuanzia 6000 hadi 10000. Soko lake ni la uhakika ukiyafikisha dar. Unaweza kuanza na kilo chache kama 10 au 15 kuangalia soko. Inalipa na hiyo pesa yako kwa biashara hiyo ni kubwa sana.

Pia unaweza kua unanunua mbuzi huko minadani unakuja kuwauza dar, mbuzi mmoja wa bei ya chini kabisa dar ni elfu 60 ambae unaweza kumnunua 20 au 25 ukijumlisha na usafiri hadi dar ni 35.

Uhakika wa soko la mbuzi dar ni wa kuaminika,ukifika hata na mbuzi 200 unawauza wote muda huo huo.

Kwa mtaji wako unaweza kuanza na mbuzi 25.

Nadhani unaweza kufikiria hvyo kama utakua una nia ya kufanya biashara.
 
Mkuu kwa dar haya madini huuzwa wapi?
 
Kama solo nilauhakika kwann abebe kiasi kidogo hivyo?..
 
Kwa kuanza maana anaenda kukutana na watu wageni kwake hivyo anaenda na kiasi kidogo,akijiridhsha anaenda na hela kubwa.

Sio vyema umshauri mtu aende na milioni 200 kwa watu asiowafaham,unaenda na kiasi kidogo ukizoea na kujiridhsha kuhusu usalama wako unaenda nazo zote.
 
Kama solo nilauhakika kwann abebe kiasi kidogo hivyo?..

Kila kitu huanza polepole ndugu sasa mtu hata hayo madini yenyewe hajawahi kuyaona then aweke pesa zote? Naunga mkono hoja ya mkuu kaka km aanze na kiasi kidogo wakati anazoea mazingira ya biashara ataongeza taratibu mbele ya safari akiwa na uzoefu na kama mambo yataenda vizuri
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom