Mtaji TZS 1 Million, naombeni ideas za biashara

Mtaji TZS 1 Million, naombeni ideas za biashara

tafuta mtu anaefuataga bidhaa china mpe akanunue smart phone kwa bei rahisi then uje uziuze mavyuoni ili mtaji uwe mkubw

Huyo wa kumwamini na kumwachia pesa asafiri nayo ni mtanzania au ni mchina? Kama ni mtanzania asijaribu hii nchi imeharibika sana watu si waaminifu hata kidogo,hata ndugu anaweza kukutapeli. Ajaribu kufanya kitu ambacho yeye mwenyewe pia atakuwa involved moja kwa moja
 
Kila kitu huanza polepole ndugu sasa mtu hata hayo madini yenyewe hajawahi kuyaona then aweke pesa zote? Naunga mkono hoja ya mkuu kaka km aanze na kiasi kidogo wakati anazoea mazingira ya biashara ataongeza taratibu mbele ya safari akiwa na uzoefu na kama mambo yataenda vizuri


kweli lakini...
 
Last edited by a moderator:
Nimehamasika na hayo madini..vipi upatikanaji wake.
Niyakwenda kukusanya kidogokidogo au inakiwaje,.ufafanuzi tafadhali
 
Kama uko morogoro au dar,nenda morogoro huko kilosa uwe unanunua madini yanaitwa feldspar uwe unakuja kuyauza dar.Unanunulia kilo moja 2000 au 2500,dar yanatoka kuanzia 6000 hadi 10000. Soko lake ni la uhakika ukiyafikisha dar. Unaweza kuanza na kilo chache kama 10 au 15 kuangalia soko. Inalipa na hiyo pesa yako kwa biashara hiyo ni kubwa sana.Pia unaweza kua unanunua mbuzi huko minadani unakuja kuwauza dar, mbuzi mmoja wa bei ya chini kabisa dar ni elfu 60 ambae unaweza kumnunua 20 au 25 ukijumlisha na usafiri hadi dar ni 35.Uhakika wa soko la mbuzi dar ni wa kuaminika,ukifika hata na mbuzi 200 unawauza wote muda huo huo.Kwa mtaji wako unaweza kuanza na mbuzi 25.Nadhani unaweza kufikiria hvyo kama utakua una nia ya kufanya biashara.
hiyo ya madini ya felspar imekaa vizuri sana ndugu...
 
Kama uko morogoro au dar,nenda morogoro huko kilosa uwe unanunua madini yanaitwa feldspar uwe unakuja kuyauza dar.

Unanunulia kilo moja 2000 au 2500,dar yanatoka kuanzia 6000 hadi 10000. Soko lake ni la uhakika ukiyafikisha dar. Unaweza kuanza na kilo chache kama 10 au 15 kuangalia soko. Inalipa na hiyo pesa yako kwa biashara hiyo ni kubwa sana.

Pia unaweza kua unanunua mbuzi huko minadani unakuja kuwauza dar, mbuzi mmoja wa bei ya chini kabisa dar ni elfu 60 ambae unaweza kumnunua 20 au 25 ukijumlisha na usafiri hadi dar ni 35.

Uhakika wa soko la mbuzi dar ni wa kuaminika,ukifika hata na mbuzi 200 unawauza wote muda huo huo.

Kwa mtaji wako unaweza kuanza na mbuzi 25.

Nadhani unaweza kufikiria hvyo kama utakua una nia ya kufanya biashara.

kwenye biashara ya mbuzi hapo sikushauri hakuna mbuz anayeuzwa elfu 25000 na usafirhadi dar...mfan moro bei ya chin minadani tena kwa wamasai tsh 45000..
 
Jiunge na fursa kutoka forever living, utaweza kutumia Tsh 910,000 tuu kama mtaji wa kuanzia na ukijituma vizuri utatengeneza mpaka zaidi Milion 3 kwa mwezi.
Kwa maelezo zaidi pm au piga 0719972458

Nina ndugu zangu wawili wa karibu Sana wanafanya hii issue. Wapo very busy and committed na forever living. Nasubiri nione mafanikio yao ndo nitaamini network marketing. Kila la kheri kwa forever living members wote.
 
Mchokoza mada hapa utapata msaada maana unachoita mtaji kwa wengine ni pesa yao ya kutumia week end. Nachoweza kukushauri fanya biashara ya umachinga hata ukianza na cover za simu
 
Utamu wa ngoma uingie ucheze usisubiri kuhadithiwa!!!

Kwa usawa huu..laki 9 uingize kwenye biashara usiyokuwa na uhakika nayo? nasubiri kwanza Nione mafanikio ya hawa ndugu zangu coz wameamua haswa kuifanya, pia nipate elimu kutoka kwao nielewe vizuri...hapo ndio nawefa Fanya maamuzi. Kwasasa hapana kabisa...mambo ya kukimbizana na cc (wenyewe wanaelewa) cjui nini..mi cyawezi bado. Hiyo laki 9 ni kianzio tu...ili ufanikiwe inabidi uwe na zaidi ya hiyo.
 
Jiunge na fursa kutoka forever living, utaweza kutumia Tsh 910,000 tuu kama mtaji wa kuanzia na ukijituma vizuri utatengeneza mpaka zaidi Milion 3 kwa mwezi.
Kwa maelezo zaidi pm au piga 0719972458

USIJARIBU HAPA!!! Tafuta biashara nyingine
 
Back
Top Bottom