Mtaji TZS 1 Million, naombeni ideas za biashara

Mtaji TZS 1 Million, naombeni ideas za biashara

Mi nafikiri hujaelewa vizur garama ya mafanikio.Kama umefuatilia huu uzi vizuri ni biashara ipi unaweza kufanya kwa mtaji wa laki 9??
Tatizo nililogundua ktk dunia ya leo, people are so negative..
Na usipochukua hatua huo uoga utaendelea kukukalia maisha yako yote!
Ondoa uoga, anza kujaribu vitu!!!

Cjawa negative babaa..nimesema nataka kuielewa vizuri kwanza ndio nipo kwenye mchakato wa kuielewa coz network marketing si sawa km biashara nyingine so cwezi kuingia kichwa kichwa. Cna tatizo na biashara yoyote mtu aifanyayo ili mradi anaielewa na inamletea faida.
 
kwenye biashara ya mbuzi hapo sikushauri hakuna mbuz anayeuzwa elfu 25000 na usafirhadi dar...mfan moro bei ya chin minadani tena kwa wamasai tsh 45000..

huko bei sana mimi nipo Tabora mbuzi bei kuanzia Tsh 20000 wale wa elfu 60000 ni yale mabeberu wakubwa kabisa ukiliona kama ndama.
ila sijajua gharama za usafiri
 
Kama uko morogoro au dar,nenda morogoro huko kilosa uwe unanunua madini yanaitwa feldspar uwe unakuja kuyauza dar.

Unanunulia kilo moja 2000 au 2500,dar yanatoka kuanzia 6000 hadi 10000. Soko lake ni la uhakika ukiyafikisha dar. Unaweza kuanza na kilo chache kama 10 au 15 kuangalia soko. Inalipa na hiyo pesa yako kwa biashara hiyo ni kubwa sana.

Pia unaweza kua unanunua mbuzi huko minadani unakuja kuwauza dar, mbuzi mmoja wa bei ya chini kabisa dar ni elfu 60 ambae unaweza kumnunua 20 au 25 ukijumlisha na usafiri hadi dar ni 35.

Uhakika wa soko la mbuzi dar ni wa kuaminika,ukifika hata na mbuzi 200 unawauza wote muda huo huo.

Kwa mtaji wako unaweza kuanza na mbuzi 25.

Nadhani unaweza kufikiria hvyo kama utakua una nia ya kufanya biashara.

Habari wakuu, binafsi nimependa iyo ya madini nataka nijaribu, msaada kwa yeyote ambae anafanya hii biashara kuhusu soko lipoje na upatikanaji wa hayo madini huko yanakochimbwa upoje? Ni mpaka yakusanywe au huwa inakuaje????

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom