Mtaji wa 10m afanye bishara gani?

peri

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
2,579
Reaction score
1,164
Habari za muda wadau?

Nina rafiki yangu ni muajiriwa serekalini.
Kapewa 10m na babake ili ajiimarishe kiuchumi.
Hajajua mpaka sasa afanye nini kwani kapewa kwa masharti kuwa afanyi biashara au chochote cha kuzalisha ila asije akaingiza kwenye mambo matumizi mengine kama pombe, wanawake nk.

Kaniomba ushauri kwani hajajua mpaka sasa afanyaje ukizingatia muda wake ni mdogo kwani anabanwa kazini na anajiendeleza kielimu na hana uzoefu wowote na biashara.

Nimefikiria kumshauri anunue gari ndogo ya biashara kama suzuki carry au hata bajaji kitu amabcho naona hakihitaji usimamizi mkubwa na kina hesabu inayo eleweka. Nimeona sio vibaya kuwashirikisha wadau wengine kwa mawazo zaidi.
Karibuni kwa michango.
 
Mkuu Kulingana na hapo kwenye red ni bora azirudishe tu hizo kwa baba yake, au baba yake ampe kwa dhumuni la kula na si kuzalisha
 
Umesmea yeye anasoma na anafanya kazi
Sasa kweli huyo baba gani anaweza kukubali mwanae amuongezee majuku ya biashara wakati akiwa anasoma.
Pili,yeye anasoma ili aje awe nani na ndoto zake ni zipi.Hiyo itamsaidia ili aweze kujenge uwezo.

Ushauri:
a)Akanunue Hisa kwnye Soko la Hisa,hapo atakuwa hana preasure,ikifika muda pesa inaingia yenyewe

b)Au anunue Carry,ambayo Hesabu yake ni Tsh:25,000 kwa siku na Bei yake hazidi Tsh:7.5m
Change itakayobakia anunue Bodaboda Moja yenye hesabu ya 7,000 - 10,0000 kwa siku ambapo bei ya haizidi 2.1m.
Kwa Maana hiyo ni kwamba ndani ya miezi kumi tu anakuwa amerejesha Pesa yote na kuanza kupata faidi sasa.

c)Pia naweza kufikiria suala la kuanzisha Mgahawa wa chakula.
Tafute eneo la watu wenye kipato cha kawaida,maana ndio watumiaji wazuri,aweke pawe pasafi na wahudum wazuri.Hapo atatengeneza pesa nzuri sana .

Yangu ni Hayo Tu.
 

Nashukuru sana [MENTION] Zanzibar Spices [/MENTION] Umeto mawazo mazuri.
Huo mtaji kampa kama njia ya kumuinua, na mzee mwenyewe nadhani hajui mambo ya shule yakoje.
Anasoma biashara, nadhani BBA open univ. Sijajua hasa malengo yake ila nadhani ni kuja kujiajiri
kwenye shuhuli zake mwenyewe kwasababu ana diplm ya ualimu ila anajiendeleza kwenye bishara.
 
Mkuu Kulingana na hapo kwenye red ni bora azirudishe tu hizo kwa baba yake, au baba yake ampe kwa dhumuni la kula na si kuzalisha

Mkuu hata ingekuwa mimi nisinge zikataa hata kama sina muda na uzoefu, ningejaribu bahati yangu.
Sidhani kama kuna mtu anaweza kukataa hela kama hiyo hasa unapopewa bure na sio mkopo.
Karibu kuchangia mkuu, ushauri ni muhimu.
 
Kampuni ya Chinaworldbuz Company Limited, tunakukaribisha kufanya biashara nasi. Wewe ni mfanyabishara, unataka inua biashara yako, unataka kupanua mipaka ya biashara yako,unataka bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na kwa bei nzuri!? Basi CWB ni mshirika wako mkuu katika bishara yako. Tupo kwa ajili ya kuipa kipaombele biashara yako na kutimiza ndoto zako!! New attempts, New possibilities.
 

fafanua kwa lugha raisi mnafanyaje biashara zenu.
 
Mh,hii kweli kali.
We utamsaidiaje mtu hata website hamna.
Email yenyewe ya kichina kweli maana yahoo hata mwanangu wa Nursery anayo.
China ! China ! China,duhh kweli ?
 
Kampuni ya Chinaworldbuz Company Limited (CWB) ni kampuni ya muungano wa vijana wa kitanzania na kichina waishio jijini Shanghai-China.Kampuni hii iliyoanzishwa february mwaka 2012 jijini Shanghai kwa Lengo la kuifikia jamii ya wafanyabiashara wa Tanzania na Africa kiujumla watakao kununua bidhaa zenye ubora wa hali ya juu kutoka nje ya nchi (hususani China) kwa ajili ya kuboresha biashara zao.Kutokana na kuwa na changamoto nyingi zinazowapata wafanyabiashara wa Tanzania katika nyanja za kukataliwa kibali cha kuvuka mipaka(VISA REJECTION), ugumu wa lugha ya kichina( LANGUAGE BARRIER),kupata bidhaa bandia (FAKE GOODS)katika masoko madogo madogo ndani ya China na pia kukosa mahusiano ya moja (DIRECT LINK) na viwanda vitengenezavyo bidhaa mbali mbali nchini China. CWB ni njia sahihi ya kuweza kuboresha biashara yako bila kukutana na changamoto tajwa hapo juu, ni rafiki mwema wa biashara yako, ni njia sahihi ya kuweza kutimiza ndoto zako katika uwanja huu wa biashara. CWB,Tunatoa elimu ni jinsi gani ya kufanya kazi na sisi, tuna toa ushauri ni aina gani ya biashara mtu anaweza kufanya kulingana na mtaji wake, tunatoa maelezo ya kina kuhusu bidhaa zetu zote tuzitoazo mfano simu, tablets,nk. Kwa Sasa makao makuu ya ofisi za CWB yapo jijini Shanghai na ifikapo January 2014 ofisi zetu zitahamishiwa Ushirika Tower jijini Dar es Salaam. Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea website yetu www.chinaworldbuz.com pia unaweza wasiliana nami kwa email juely2006@yahoo.com au justineluvanda@gmail.com, simu namba +8613524159707.
Usiwe na shaka kuuliza au kuhitaji mafafanuzi ya kina. Tupo kwa ajili ya kufikia mahitaji ya wafanyabiashara na watu wanaotaka kufanya biashara.
Asanteni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…