Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aiseee[emoji112][emoji112][emoji112][emoji112]monopoly inc Cacs le zombie nitaelezea kwa kifupi niliwezaje kuanza biashara bila mtaji,
Nilikuwa kwenye kipindi kigumu kidogo kimaisha na bahati mbaya simu yangu iliharibika na kuitengeneza ilikuwa ni laki 2 sikuwa na hiyo pesa,mwanangu alikuwa na iPad nayo akavunja kioo,katika kuhangaika nikapata wazo la biashara ugumu ukaja nitafanyaje iyo biashara ilihali sina mawasiliano,nikaamua kuanza kibishi nikaomba simu ya mtu nika login kwenye account yangu insta nikabadili kuwa ya biashara na jina,nikaingia kwenye account ya mama namfahamu tuu ana duka kkoo la nguo nika screenshot picha nikaziweka kwenye account yangu nikaanza kutangaza biashara kwa kasi nilikuwa nalike na kucoment kwenye account maarufu ivo ivo kwa kuazima simu na namba ya simu ambayo wateja walikuwa wakipga niliomba kwa mtu alikuwa na kitoch kaweka laini moja ndo na mimi nikaweka yangu ikawa mtu akipga ananiita,bahati nzuri wiki ya kwanza nikapata wateja sita wa mikoani na mmoja wa dar alikuwa anataka vitu vingi,nikawa navizia hawa wamikoani wakituma hela ndo niende nikamchukulia uyu wa dar nimpelekee akinilipa ndo niende nikawachukulie hawa wa mikoani niwatumie vitu vyao,wa mikoani wakawa wana delay kutuma pesa na wa dar anataka mzigo wake ikabidi nizame kkoo niongee na yule mama akakubali kunipa mzigo kwa mali kauli,nashukuru yule mteja ndo alinifanya nipate mtaji wa kuendelea basi yule mwenye kitoch kumbe kilikuwa sio chake nikachukuliwa basi kuna dada akanipa kitoch cha ofisini kwao nitumie kwa muda,wateja wakaanza kusema nafanyaje biashara bila WhatsApp nikajikongoja pamoja na vikwazo na changamoto nilizokuwa naoi ndani ya mwezi nikanunua smartphone na mtaji ukawa umekua sana kwa sababu nilikuwa nafanya juu kwa juu sina frem
Aiseee[emoji112][emoji112][emoji112][emoji112]
Asante sana mkuu, kumbe fursa ni nyingi tu sema namna ya kuzifikia ndo tunapofeli.
tutajua kimakubaliano mkatabaAkishindwa kurejesha,mfano akapata hasara..
Ufanyaje mkuu??
NAKOPESHA NA RIBAMkuu na mimi ninaomba uniazime mtaji maana nimekwama kabisa.
huna ndugu wa kukuamini akupe hata50k au uza simu kama smartphone nunua Nokia tochi utakujanunua nyingine mbeleniHeshima kwenu nyote.
Nina uhitaji wa kufanya biashara ndogondogo ila tatizo mtaji sina hivyo wadau mwenye kazi yoyote naomba anipatie ili nipate mtaji wa kuanzia. Kazi yoyote ya malipo kwa siku au week ingependeza zaidi.
Nawasilisha