Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nashukuru sana kaka kwa ushauri wako.be blessedMkuu kimsingi mimi ni mwanafunzi kama ww, na nimeshawahi kujaribu kugusa baadhi ya biashara ikiwemo kibanda cha chipx ambapo uendeshaji wake unauhuiano mkubwa na mgahawa, mind you rafik yangu, pesa ya mkopo sio ya kuanzishia biashara risk km ya mgahawa ukizingatia bado unasoma, biashara ya mgahawa inakuhitaji kuliko ww unavyoihitaji, huwezi ukafanikiwa katika biashara hiyo kwa kuachia watu waiendeshe,
Naweza nikasema asilimia 90 ya biashara yoyote ambayo unaanzisha halaf hauna muda wa kua karibu nayo utapoteza pesa yako ukizingatia ni pesa ya mkopo, binafsi kwa uzoefu wangu dnt the risk, biashara ya chakula kuna siku unaweza ukaamka wafanyakaz wamegoma kuja kazini ww upo chuo unafanyaje?
Jitafakar tena kisha fanya utafiti wa kina ndg yang,
Sasa ni biashara gan ambayo naweza nikakushaur ufanye? 1. Uuzaji wa magodoro, biashara hii hata ukiwa unasoma moshi yenyewe ipo dar mtu hawezi kukuibia ingawaje unatakiwa uweke mtu ambae hana uwezekano wa kukimbia na mtaji.
2. Biashara ya vinywaji, vya jumla, biashara hii hata ukimuweka mtu ukaendelea kusoma bidhaa zake zinahesabika na ni ngumu kukuibia, ingawaje hii itakuhitaji katika kuweka mbinu za masoko, za mauzo na promosheni mbalimbali,
3. Furniture, hii ni biashara ambayo unaweza ukaanza nayo kwa mtaji mdogo lkn ukakua kdg kdg na biashara hii hata ukiendelea kusoma ukaweka mtu furniture zitauzika 2 na mahesabu utakua nayo mkononi.
4. Usafiri, hapa namaanisha bajaji, tafuta kilema mnunulie bajaji muwekee pale posta feli utapiga pesa bila stress nyng kichwan ingawaje ukiweka mtu muhuni hii biashara utaijutia sana, tafuta mtu makini, na mwaminifu mkuu..
Mwisho katika kila biashara utafiti, utafiti, utafiti ni muhimu sana, usikae kuchat na kushinda instagram nenda kazungumze na watu huko nje, fanya utafiti wa biashara inayokuvutia kwa watu ambao tyr wanazo n. K itakusaidia sana
Asante kaka.Tenga TZS 128,500 wekeza kwenye mradi wa Rifaro. Zinginezo wekeza kwenye mradi utakaoamua kuufanya. Ni vyema kuwa na biashara tofauti wakati mmoja ili kupunguza risk ya kuwekeza kwenye mradi mmoja kwani ukishindikana basi na mtaji wako wote umekwenda.
Biashara ya kuwekeza kwenye mradi wa Rifaro haina gharama zingine zaidi ya kulipia mtaji wa TZS 128,500 tu na ni biashara ambayo hata kama uwe mzito kiasi gani huwezi kupata hasara kwani lazima hela yako itarudi kadri siku zinavyokwenda.
Kwa maelezo zaidi kuhusu mradi huu wa Rifaro, soma thread hii
Kwa nini utumie simu yako ya mkononi bila kulipwa wakati kuna Rifaro?
wewe acha mambo ya ajabu....hizo product weka humu tuzidadavue usije ukawa unataka kumuingiza mkenge na milion zake hizo tena za mkopoWasiliana nami kuna priduct itakutoa come and see 0786741162
Mkuu hongera kwa ushauri mzuri na unaotia moyo lkn kwa manufaa ya wanajamvi nina maswali mawili kutoka ktk ushauri wako mkuuNdugu kwanza hongera kwa ujasiri na uamuzi uliochukua wa kutaka kuwa mjasiliamali.Labda kwa kukushauri tuuu,hiyo biashara wala usiogope kuifanya yaan ianze fasta na usisite chochote, watu wengi wanaogopa kuwa wajasiliamali kwa sababu ya risk.lakini amini usiamini HAKUNA BIASHARA YOYOYTE DUNIANI ISIOKUWA NA RISK NA KUPATA HASARA NI JAMBO LA KAWAIDA!!!
Fanya iyo biashara fasta ili ikupe experience ya kupata hasara na ikukomaze ili upate ujasiri wa kuwa risk taker...ngoja nikupe historia yangu kidogo may be unaweza ukajifunza kitu;
miaka mi 4 iliyopita nilipata kamtaji kangu kidogo tu na nikawa na dream ya kuanza biashara ya kusupply matunda katika soko moja,hivyo niliwaza sana naanzaje kuingia katika biashara hii,huwezi amini pamoja na personality niliyokuwa nayo nilichukua maamuzi magumu sana ambayo hata mke wangu kipindi hicho hakujua kwanini niliamua kufanya vile,nilivizia fuso moja linaloleta matunda pale sokoni nikaomba kuwa tanboy bila ya malipo yoyote yale,dereva alinikubalia na nikaanza kupiga mzigo kama kawa,fuso naenda nalo shambani tunapakia mzigo tunaleta sokoni tunashusha tunauza,ivyo ivyo mtoto wa kiume ndo ikawa mchezo wangu wa kila siku..Kichwani nilikuwa najifunza mengi na kupata experience ya biashara ile..Kwenda na fuso shambani (ilinipa mwanya wa kufahamiana na wakulima,bei ya kununulia pamoja na connection zote za source ya matunda yangu), Kusafirisha mzigo na fuso hadi sokoni (ilinipa mwanya wa kujua gharama za usafirishaji na changamoto zake njiani)..kushusha mzigo sokoni ( nilipata mwanya wa kuwafahamu wanunuzi wa matunda,bei ya manunuzi n.k) Baada ya miezi 6 ya kuteseka na utanboy bila kulipwa ndipo nikaanza rasmi kazi iyo,aiseee nilikuwa natirirka tuuu maana nilikuwa nimeshaifahamu nje ndani na connection za wadau zote ninazo na nilikuwa tayari nimeshajenga urafiki nao.. Leo hii naandika haya nipo mbali sana na inshallah mungu akijalia mwezi wa 5 ntakuwa namalizia deni langu nililochukua benk kwa ajili ya kununua fuso langu mwenyewe. Namshukuru mungu saivi namimi namiliki shamba langu mwenyewe,fuso langu mwenyewe na nimetoa ajira pia kwa vijana wengine.
Kila la kheri katika uamuzi wako mkuu,USISITE ANZA SASA NA DREAM BIG,BAADA YA MIAKA KADHAA HUENDA UKAMILIKI HOTEL KABISA.Mungu akusaidie.