MTAJI wa ML 50,

MTAJI wa ML 50,

na akifa kabla hizo bonds hazijamature? atakua amepoteza jasho lake la miaka yote hiyo. namshauri aile tu hiyo hela au awakopeshe watoto wake wakafanye biashara then kila mwisho wa mwezi wanamtumia marejesho pamoja na riba.
 
Katika hali ya kawaida na pia in finance theories, bond ndio biashara regarded km yenye risk ndogo kabisa ukilinganisha na biashara zingine, ila kwa kuweka bond kiinua mgongo ni kutafuta unnecessary flustrations na kuyakaribisha mapema magonjwa ya uzeeni especially kwa style ya uendeshaji wa serikali kama hii yetu iliyojaa usanii. Fanya biashara ya bond kwa hela ambayo ni ya excess na isiyo ya mawazo km hii ya kiinua mgongo.
 
Hakuna kosa kubwa kama kuanza biashara unapokuwa umestaafu. Hizo mil 50 zitaisha zote. Biashara ina changamoto nyingi sana. Hataweza kuzihimili. Nashauri atafute wataalam wa kumsaidia, lakini hata hili gumu, yaani sijui afanye nini. Alitakiwa ajiandae mapema atakapokuwa amestaafu atafanya nini. Kwa sasa naona kama kachelewa sana. Biashara sio lelemama ndio maana sio kila mtu anaweza kuifanya.QUOTE=Yegoo;6083939]Heshima kwenu ndugu!! Nina mjomba wangu anastaafu mwaka huu! Na pensheni yake itasoma kama Mil 50,hivyo wadau Naomba mchangunuo wenu Wa biashara gani afanye!!![/QUOTE]
 
Soko la hisa hapa kwetu bado halijaendelea. Ulaya watu wanafaidika na hisa kwa kununua zikiwa bei ndogo na kuziuza zinapokuwa zimepanda. Yaani wana "speculate" kuwa zitapanda baadae. Huwezi kupata hela nzuri kwa kutegemea gawio kwani huwa ni hela ndogo sana. Nisingekushauri ununue hisa. Kwa mfano hizo mil 50 ni kama hisa 50,000 kama kila hisa inauzwa 1000. Gawio hutolewa kama kampuni imepata faida na huwa kidogo sana kwani fedha nyingine lazima zibaki kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kampuni. Nilinunua hisa za TOL mpaka leo hakuna gawio na hisa hizo zimeshuka bei hivyo hata mtu akiuza atapata hasara. Nilinunua hisa za TBL zilipotangazwa tu hisa 100 kwa shs 50,000 na niliziuza zilipokuwa 1500 nikapata 150,000. Ningesubiri hadi leo ningepata zaidi. Hata hivyo kwa Tanzania unasubiri sana na ukiweka mfumuko wa bei na mambo mengine sijui kama kuna faida yoyote. Upande wa hisa sikushauri.
mkuu vipi kuhusu hisa za crdb na faida gani waweza pata per hisa kwa mwaka?
 
Guys wazee wetu wengi hawavuki miaka mitano wanakufa! Tatizo kubwa ni kukosa maandalizi ya kustaafu. Siku unayopewa barua ya ajira ndio mwanzo wa maandalizi ya kustaafu. Kimsingi huwezi kuanzisha biashara baada ya kustaafu bali kuiendeleza! Mzee aondokane na pressure anunue hisa DSE ktk hali ya kawaida mstaafu akipata sh. mln 1 ataishi siku zake bila hofu.
Tuwasiliane for further consultation
 
Natamani hizo pesa nizikamate mimi,hata nusu yake tu zingenitosha kuanzisha duka la kuuza cement,na vifaa vingine vichache vya ujenzi kwa kuwa site niliyokuwepo inaniruhusu kufanya hivo.
Lakini kama wengi walivyochangia,biashara inahitaji uzoefu,zipo changamoto na fursa katika biashara ambazo baadhi huwezi kuzitambua hadi uingie kwenye biashara.
Najaribu kumfikiria huyo uncle wako,iwapo anaanzisha biashara kwa muda wa, say miezi miwili haoni mapato kama alivyotarajia,ataweza kuvumilia au ndo atapata stroke kabisa kuhisi amepata loss...!
Kwa kifupi,anatakiwa kwanza apate watu wakumshauri namna nzuri ya kuendesha biashara,misingi na miiko yake. Ajue kabisa kuwa akifungua biashara,yeye ni mtumwa,siyo bosi. Kwamba hizo pesa zisimfanye aonekane bosi. Ataonekana anadharau na atapoteza wateja.
Tafuta post za Sacha (kama nimekosea kuandika jina nisamehewe) humu jf na wadau wengine,wanamichango muhimu sana.
 
Natamani hizo pesa nizikamate mimi,hata nusu yake tu zingenitosha kuanzisha duka la kuuza cement (kuna post zinazohusu cement za Pakistan,zilinivutia),na vifaa vingine vichache vya ujenzi kwa kuwa site niliyokuwepo inaniruhusu kufanya hivo.
Lakini kama wengi walivyochangia,biashara inahitaji uzoefu,zipo changamoto na fursa katika biashara ambazo baadhi huwezi kuzitambua hadi uingie kwenye biashara.
Najaribu kumfikiria huyo uncle wako,iwapo anaanzisha biashara kwa muda wa, say miezi miwili haoni mapato kama alivyotarajia,ataweza kuvumilia au ndo atapata stroke kabisa kuhisi amepata loss...!
Kwa kifupi,anatakiwa kwanza apate watu wakumshauri namna nzuri ya kuendesha biashara,misingi na miiko yake. Ajue kabisa kuwa akifungua biashara,yeye ni mtumwa,siyo bosi. Kwamba hizo pesa zisimfanye aonekane bosi. Ataonekana anadharau na atapoteza wateja.
Tafuta post za Sacha (kama nimekosea kuandika jina nisamehewe) humu jf na wadau wengine,wanamichango muhimu sana.
 
try kuby Bajaj na utafute sehem ambayo haitaichosha hiyo Bajaj na uanze kupga hela
 
mbongo akisikia arufu ya pesa vinyweleo vinamsimama.
 
Back
Top Bottom