Natamani hizo pesa nizikamate mimi,hata nusu yake tu zingenitosha kuanzisha duka la kuuza cement (kuna post zinazohusu cement za Pakistan,zilinivutia),na vifaa vingine vichache vya ujenzi kwa kuwa site niliyokuwepo inaniruhusu kufanya hivo.
Lakini kama wengi walivyochangia,biashara inahitaji uzoefu,zipo changamoto na fursa katika biashara ambazo baadhi huwezi kuzitambua hadi uingie kwenye biashara.
Najaribu kumfikiria huyo uncle wako,iwapo anaanzisha biashara kwa muda wa, say miezi miwili haoni mapato kama alivyotarajia,ataweza kuvumilia au ndo atapata stroke kabisa kuhisi amepata loss...!
Kwa kifupi,anatakiwa kwanza apate watu wakumshauri namna nzuri ya kuendesha biashara,misingi na miiko yake. Ajue kabisa kuwa akifungua biashara,yeye ni mtumwa,siyo bosi. Kwamba hizo pesa zisimfanye aonekane bosi. Ataonekana anadharau na atapoteza wateja.
Tafuta post za Sacha (kama nimekosea kuandika jina nisamehewe) humu jf na wadau wengine,wanamichango muhimu sana.