miamiatz
JF-Expert Member
- Dec 4, 2017
- 505
- 941
A friend of mine aliguswa na makala yangu ya biashara ya nafaka kwa wenye mtaji mdogo. Alipoguswa akaamua kuingia kwa akiba yake ya TZS 10M aliyokuwa nayo benki.
Akanunua gunia 300 kwa wastani wa TZS 30,000 kwa gunia. Alitumia TZS 1M kwenye madawa na usafiri. Alikuwa na room aliyoiita ya wageni pale home kwake japo room hiyo ilikuwa ikipata wageni mara chache sana.
Aliigeuza room hiyo kuwa store ya mahindi aliyonunua. Mengine akayaweka kichumba kilichoitwa store na mengine akayajengea kisehemu cha kuhifadhia ndani ya fence ya nyumba aliyopanga.
Alinunua baada ya mavuno July mwaka jana 2019 na miezi sita ikapita wiki iliyopita alienda sokoni na akuliza bei ya mahindi na kuomba kusupply gunia 300. Bei ya rejareja ilifika TZS 750 kwa kilo. Bei ya jumla akauza TZS 650 kwa kilo.
Jamaa akajipatia TZS 19.5M ikiwa ni TZS 9.5M zaidi ya pesa aliyotumia kununua yale mahindi. Anasema faida yake anahesabu hiyo TZS 9M mana kuna matumizi tumizi yalimbidi kulipia pale sokoni japo haikufika TZS 500,000.
Ongezeko la TZS 9M ni sawa na wastani wa ongezeko la TZS 1.5M kwa mwezi. Sio wote tufanye hii ila kwa wale wachache hata kama una TZS 30M we nunua gunia zako 1000 July ijayo Mungu hamtupi mja wake. Penye jitihada ndipo penye mafanikio.