Mtaji wa tzs milioni 10 biashara kwa wale walio busy sana yenye faida ya tzs 1.5m

Mtaji wa tzs milioni 10 biashara kwa wale walio busy sana yenye faida ya tzs 1.5m

Kwa mawazo haya mkuu, utatafuta mchawi wa maendeleo yako kumbe ni wewe!!!! Ndio maana wengi waliofanikiwa ktk ujasiriamali ni wale hata shule hawakwenda/hawakufika mbali, wao risk sio inshu, lakini nyie ma prof. Utachukua calculator fomula nyingi, risk assessment,*fire/floods=project not viable
Aisee hiyo formula ya risk assesment imenichekesha sana. Na kweli kwenye biashara ndivyo walivyo wasomi wengi. Akiweka formula kama hiyo uliyoandika kwenye calculator anajikuta anaogopa kila biashara.
 
Najua,lakini kama mtu upo serious kweli gunia 300 ni nyingi mno kuziweka home kwenye risk kubwa.

Weka hata godown za mashineni wana bima na kama ni mpunga hawakutozi hata storage isipokuwa unatakiwa ukobolee mashineni kwao na pumba uwaachie
Sawa ndugu nimekusoma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
There you go...!!! Contributions r better than criticisms..!!!
Najua,lakini kama mtu upo serious kweli gunia 300 ni nyingi mno kuziweka home kwenye risk kubwa.

Weka hata godown za mashineni wana bima na kama ni mpunga hawakutozi hata storage isipokuwa unatakiwa ukobolee mashineni kwao na pumba uwaachie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo maana Motivational speakers wanapiga pesa daily na kuneemeka na hesabu za vilimo vya kwenye makaratasi huku vijana wakiambulia hasara kwenye kilimo na ufugaji kisa wanaangalia faida tu.

Badala ya kupewa ukweli wa changamoto zilizopo wanaambiwa hawawezi kufanikiwa bila ku-TAKE RISK! Yaani wewe lima/fuga tu mambo ya soko ifanye iwe risk yenyewe!

Kama kuna mfanyabiashara wa mazao SERIOUS kabisa na anahifadhi gunia 300 kwenye chumba cha wageni nyumbani kwake karne ya 21 HE'S/SHE'S A LOSER! Hiyo biashara ya kuficha mazao kusubiri bei yenyewe iko ukingoni kwa sasa hamasa ipo kwenye kuongeza thamani zaidi.

Shida humu wengi ni pigheaded (ukiwaonesha kitu kwa kidole,wanang'ang'ania kuangalia kidole chako) yaani huo mfano wa risk ya moto ndo umechukuliwa kama the only risk ilhali kuna majanga chungu nzima.

Kwa sasa wenye akili timamu wamekuja na bima ya mazao yangali shambani halafu mtu anakuhamasisha uweke gunia 300 sebuleni sababu mafanikio ni ku-take risk.

Wekeni na pesa zenu chini ya mito basi msipeleke bank ili mfanikiwe zaidi kwa ku-take risk!
 
Biashara ya Kuweka Stock ya Mahindi haitabiriki Kuna Mwaka itakiwa Nzuri na kuna Mwaka inakuwa sio Nzuri sana ila kukukata sio rahisi kama hukuwa mzembe ,inatakiwa ukae ktk biashara hiyo ili Mazuri yakukute pia Mwaka mbaya uwe changamoto kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: amu
Kwa mawazo yako haya bila shaka wewe utakuwa ni msimamizi wa godown mojawapo linalomilikiwa na mume wa dada yako
Amekupa kazi kukunusuru na ujobless hivyo uko hapa kutafuta wateja Karne,
 
Kwa mawazo yako haya bila shaka wewe utakuwa ni msimamizi wa godown mojawapo linalomilikiwa na mume wa dada yako
Amekupa kazi kukunusuru na ujobless hivyo uko hapa kutafuta wateja
Rubbish
 
Karne uko sahihi lakini tatizo ni jinsi unavyowakilisha hoja yako. miamiatz kwenye maelezo ya mfano alioutoa huyo jamaa ndio kwanza anaanza hii biashara kwa sasa. Kila jambo lina ugumu wake na makosa mengi unapoanza mwanzoni. Uzuri umesema kabisa mambo ya kuhifadhi mazao ndani mlifanya zamani sana. Kwakuwa huyu ndio anaanza, hii ndio zamani yake. Kadri siku zinavyoenda hataweka tena ndani, atakua ana mtaji mkubwa wa kununua mazao mengi zaidi, atajifunza mbinu za kuongeza ufanisi, kuepuka gharama zisizo na ulazima n.k

Nafikiri badala ya kubezana na kutumia lugha za kejeli, tungeweza kujifunza hapa tukafaidika wote kwa hili jukwaa.

Mbona wapo matajiri wanaweka pesa nyumbani mkuu, tena wengi tu.
 
The Monk huu mjadala umeharibiwa na hao waliokuja na jazba zao from nowhere.

Ungeuona uzi kabla haujahaririwa na kufutwa comment za matusi pengine huo uwasilishaji wangu usingeutilia shaka.

Mkuu nimekupata vizuri sana. Mitazamo ya watu inatofautiana sana. Huu uzi ungetumika vizuri kwa watu kuona fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo hususan mazao.

Unaweza kuwa na eneo lako Dar badala ya kulitelekeza ukajenga godown watu wakahifadhi mazao. Pia kuna watu wa bima wanaweza kuona namna gani waboreshe huduma zao kukidhi haja ya hili soko. Cha msingi jazba na mihemko tuviweke kando.

Naamini sana kujifunza kupitia kwa watu wenye uzoefu wa kufanya jambo.
 
Huyo wa Nyumba kuungua nafananisha na Jinsi waliokuwa tunatishwa cheza tu Mpira uvunjike ndio ujue vyema.

Leo hii wale tuliocheza nao hata hatufanani..na mmoja wao katika kundi anajulikana sana.

Unagopa Nyumba kuungua ....basi tusingeisha kwenye Nyumba.

Nyumba iungue kisa Mahindi yapo ndani.Labda ana mawazo ya kwenda kumchomea next time
 
Back
Top Bottom