Wadau what matters is not how much you have,but how do u spend the litle you have.4million ni pesa nyingi sana.Unapasawa kuchagua aina ya biashara amboyo mtaji huo unakidhi.Mfano wa biashara hizo ni:
-fundua duka la usambazaji mikate.
-huduma za MPESA/TIGO PESA/ZPESA NA AIRTEL MONEY.
-Mradi wa ufugaji kuku wa nyama,endapo unaeneo lenye kukidhi mradi huo.
-BBQ na huduma kama ziambatanozo na biashara hii.
-Tafuta vijana waaminifu ununue mashine za kutengeneza bisi maeneo yaliyo na watu wengi.
-Nunua Mchele msimu wa uvunaji uulete DSM utauza baada ya miezi miwili au mitatu na utatengeneza faida.
NB Shughuri hizi na nyingine nyingi zinafana zikitendwa na mtu asiye nia makuu kwa haraka,pia zingatia uwezo wako utokao ndani ya moyo wako.usifanye biashara usiyo na furaha nayo eti kisa wengi tumekushauri hivyo.Ni jukumu lako wewe na mwenzi wako kuchagua nini mfanye mkizingatia mazingira yanayo wazunguka.
nakutakia ushindi na mafanikio tele pale utakapo ridhia shughuri ya kufanya,nami niliwahi pita huko lkn sasa nimeinuka,Mungu atakuinua na wewe songa mbele pasipo hofu.