Mtaji watu na Uchumi wa Kati Tanzania

Mtaji watu na Uchumi wa Kati Tanzania

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Leo nitajaribu kuandika katika namna ambayo nitakayoyandika yatakuwa yanatawaliwa kwa kiasi kikubwa na nadharia ya uwekezaji kwenye raslimali watu kwa sababu ya umuhimu wake hasa wakati huu ambapo ndiyo kwanza tumeanza kuelekea kwenye shauku ya Taifa letu yaani kukua kiuchumi na kufikia hatua ya uchumi unaoongizwa na viwanda.

Nadharia hii iliasisiwa mapema sana na wabobezi wa masuala ya uchumi akiwemo Adam Smith katika karne ya 17 lakini haikutia uzito sana kwenye watu mpaka mwazoni mwa miaka ya 1960's katika shule ya Uchumi ya Chicago waliibuka wataalamu kama Mincer,Garry Beker na wengineo na kuyaona mapungufu ya wataalamu wenzao wa awali kisha kuboresha nadharia hii muhimu ambayo leo imekuwa chachu ya ukuaji wa mataifa lukuki Duniani.

Kwa tafsiri nyepesi kabisa nadharia hii inaelezea mtaji watu kama jumla ya mawanda yote yanayohisisha maarifa ujuzi na uwezo unohitajika katika maisha na kazi,mawanda ambayo hujengwa na elimu bora.Mtaji watu unaweza kujitikeza katika mazingira yoyote yale yanayoweza kuinua tija au uzalishaji wa mtu.

Kinachoufanya nguvukazi au watu wanaofanyakazi kutofautiana katika uzalishaji na mapato yao ni kila kitu kilichopo ndani yao mfano uzoefu, mafunzo, akili, nguvu na bidii ya kazi.

Kwa mujibu wa maandiko mengi yanayogusa uchumi yanaonesha karne ya 21 ikishuhudia mabadiliko makubwa ya uzalishaji katika uchumi yakihamia kwenye mitaji ya kifizikali " physical asserts" kama ardhi,mitaji mingine ya pesa kwenda kwenye mitaji mingine isiyoyakifizikali au isiyoshikika mathalani maarifa,ujuzi bidii,afya n.k.

Uchumi wa karne ya 21 unajikita zaidi kwenye maarifa " knowledge economy" hivyo unahusisha zaidi vitu visivyoshikika ambavyo nguvu kazi (watu) wanapaswa kuwa navyo katika maeneo wanaofanyia kazi.

Kwa mfano yapo maelezo mazuri sana yaliyo waki kutolewa na Benki ya Dunia mwaka 2015 "..ni vigumu sana kwa Taifa kukua ikiwa watu wake ni dhaifu na wagonjwa".Hii inadhihirisha kuwa Taifa linahitaji kuwekeza kwenye uwezo na afya za watu wake kama kinataka kuendelea kuwepo.

Mwezi Octoba mwaka 2018 Benki ya Dunia ilizindua kipimo cha mtaji watu kilichoitwa" Human Capital Index(HCI).Kipimo hiki kiliandaliwa kuweza kuonesha takwimu za kimahesabu za mchango wa afya na elimu kwenye uzalishaji wa Taifa katika kizazi cha pili cha nguvu kazi ya Taifa.Kipimo hiki kiliandaliwa kuweza kupima mtaji watu wa mtoto anayezaliwa mpaka atakapofikisha miaka 18.Viashiria vilivyoambatishwa kwenye kipimo hicho ni vitano ambavyo ni:1.Kuishi kwa watoto,2.Uandikshwaji wa watoto shuleni,3.Ubora wa elimu, 4.Ukuaji wa Afya na, 5.Kuishi kwa watu wazima.

Nchi 157 zilihusishwa katika kufanya majaribio ya upumuaji wa mtaji watu ambapo Nchi zilizoendelea zilionekana kuwa na kipimo cha mtaji watu kilichozidi 0.75, India 0.44.Na Nchi ya Singapore ndiyo iliyokuwa na mtaji watu mkubwa kuliko mataifa mengine yote yaliyopimwa huku Amerika ikishika nafasi ya 24 na Uingereza ikiwa ya 15.

Nchi za kusini mwa Asia na kusini mwa janga la Sahara (Tanzaia ikiwemo)zilionekana kuwa a kiasi kidogo sana cha mtaji watu.Nchi nyingi za Afrika zina huduma duni ya elimu(formal education).

Tahadhari iliyotolewa na Benki ya Dunia kwa Nchi zenye mtaji watu mdogo ni kwamba wimbi la matumizi ya vifaa vya vinavyoongozwa na compyuta(automation) linaweza kuathiri sana Nchi hizo kwa kupunguza ajira.

Nikiwa mmoja wapo wa watoto wa Tanzania imefarijika kushuhudia Taifa langu likiingia kwenye uchumi wa kati uliokuwa sehemu ya ndoto za wasisi wa Taifa hili ambao hawajaweza kuona kama tunavyoona leo ila walikuwa na ndoto ya tunachokiishi leo.

Tanzania chini ya uchumi wa kati inahitaji uwekezaji mkubwa na wa dhati kwenye mtaji watu katika kipindi hiki kuliko kipindi chochote kile sababu ndilo hitaji mahususi la kumbo la wakati tulio (tunaouishi).

Viashiria hivi vimenisukuma kulionesha hili ili matunda ya uchumi wa kati yasiwe ni jambo la kifikirika kwetu ila yawe na tija kwetu na kwa vizazi vijavyo kwa sababu uwekezaji kwenye watu ni kama uwekezaji wa kibiashara unaotazamia mrejesho(returns).

Rai yangu ni viongozi wote katika nafasi yoyote kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha tunaendana na kumbo na uhitaji wa wakati tulionao kwa kuwekeza kwenye watu au mtaji watu.
 
Watu ni kweli rasilimali lakini hao watu lazima uwe umewaaandaaa,sio kama sisi wengi wao hawajaandaliwa na hata walioandaliwa elimu yao iliyowaandaa mbovu kupindukia na kuwafanya wafanane na hao wasioandaliwa.

Bahati mbaya hatujawahi pata viongozi wa kuweza kuaandaa vyema rasilmali watu ili taife lisogeee,wote wapiga porojo na kujinufaisha basi
 
Watu ni kweli rasilimali lakini hao watu lazima uwe umewaaandaaa,sio kama sisi wengi wao hawajaandaliwa na hata walioandaliwa elimu yao iliyowaandaa mbovu kupindukia na kuwafanya wafanane na hao wasioandaliwa. Bahati mbaya hatujawahi pata viongozi wa kuweza kuaandaa vyema rasilmali watu ili taife lisogeee,wote wapiga porojo na kujinufaisha basi
Jitihada zipo ila tunahitaji viongozi wetu wadhamirie kwa dhati kabisa kuwekeza kwenye mtaji watu.
 
Back
Top Bottom