Mkuu Malila, hicho unachokisema kinaweza kisiwe kweli. Watu wa animal production ni wengi kuliko animal health! Iko hivi,, kule mitaani hata mwenye diploma ya General Agric. naye huwa anajiita mtaalam wa afya ya mifugo, mtu mwenye diploma ya Animal production naye anajiita wa animal health. Ila kwa sasa baada ya vyuo vya mifugo kuwa chini ya wakala wa mafunzo ya mifugo diploma zote mbili zimeunganishwa na kuwa Diploma in Animal Health and Production (DAHP) wakati zamani tulikuwa na DAH pamoja na DAP. Ilikuwa inajulikana tangu zamani kwamba masomo ya DAH ni magumu kuliko ya DAP sasa watu wengi wakawa wanakimbilia huko kwenye DAP kukwepa msala wa DAH (sijui mambo ya anatomy and physiology, biochemistry 1 & 2, systemic anatomy, medicine 1 & 2, meat hygiene and inspection n.k.) na ndo maana hawa jamaa wako wengi kuliko watu wa DAH tofauti na ulivyosema hapo juu. Shida inayochanganya watu kule mitaani ni kule kuwatofautisha hawa jamaa, inakuwa ngumu sana maana kila mmoja anajitahidi kujitambulisha kwamba yeye ni DAH ili apige hela za wafugaji. Ila sisi wenyewe tunajuana!! Pia tangu zamani vyuo vilivyokuwa vinatoa diploma ya animal production vilikuwa vingi kuliko vya animal health (mfano DAP ilikuwa inapatikana Tengeru, Mpwapwa, Morogoro, Madaba na Buhuri) wakati DAH ilikuwa Tengeru na Mpwapwa (kwa idadi kubwa - max 70 per year @), Morogoro na Madaba (idadi ndogo kabisa).