Usihangaike na "waosha nyota" wa dunia hii ambao wanakwenda kuichafua au kuiba kabisa nyota yako! Safisha nyota yako kwa Damu ya Yesu Kristo. Ukiwa unaoga chukua maji na jimwagie huku ukisema, Nasafisha nyota yangu kwa Damu ya Yesu Kristo. Rudia angalau mara 3, fanya hivyo kila wakati, sema; Nasafisha mwili wangu, roho na nafsi kwa Damu ya Yesu Kristo... Nasafisha maisha yangu kwa Damu ya Yesu Kristo, naondoa uharibifu wote wa kichawi na kiganga dhidi yangu, kazi yangu, familia yangu, mali zangu, etc. Sema mara nyingi kila wakati. Kama una imani utaona mambo yako yatakuwa sawa na mikosi itaondoka. Endelea kuchapa kazi manake mafanikio ni KAZI NA SALA!