Helikopta mbili zimegongana wakati zikijiandaa kutua katika eneo la Mlima Everest nchini Nepal.
Mtalii mmoja kutoka India amefariki dunia, huku raia mmoja wa New Zealand akiokolewa baada ya ajali hiyo.
Ajali hiyo imetokea wakati huu ambao ni msimu wa kilele wa watalii wanaokwenda kufanya matembezi ya milimani katika wilaya ya Solukhumbu, eneo linalopatikana karibu na Mlima Everest nchini Nepal.