Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 9,397
- 12,415
Habari za leo wakuu,
Natumai mpo salama na mnaendelea vizuri.
Gesi ya kaboni dayoksaidi (CO₂) imekuwa ikitolewa kwa wingi sana kutoka kwenye injini za magari pamoja na mitambo ya viwandani. Mara tu mafuta yanapochomwa ndani ya injini au mitambo hiyo, huzalisha gesi mbalimbali, ambapo moja kuu ni kaboni dayoksaidi.
Mbali na CO₂, pia kuna gesi nyingine zinazotolewa kama vile oksaidi za nitrojeni, dinitrojeni oksaidi, methane, pamoja na hidrokaboni nyingine. Gesi hizi zote huingia kwenye anga la hewa kila sekunde, na kusababisha kuongezeka kwa uchafuzi wa mazingira kwa kiwango kikubwa.
Hata hivyo, kati ya gesi zote hizo, kaboni dayoksaidi ndiyo inayozalishwa kwa wingi zaidi, jambo ambalo limepelekea kuongezeka kwa kiasi chake kwenye anga. Gesi hii ni mojawapo ya sababu kuu zinazochangia ongezeko la joto duniani (global warming).
Kutokana na changamoto hiyo, wataalamu mbalimbali duniani wamekuwa wakibuni mbinu tofauti za kupunguza au kudhibiti utoaji wa gesi ya CO₂. Baadhi ya mbinu hizo ni pamoja na kuikusanya gesi hiyo na kuihifadhi kwenye matenki maalum au kwenye miamba chini ya bahari (carbon capture and storage). Hata hivyo, njia hizi zimeonekana kuwa na gharama kubwa na wakati mwingine ufanisi wake huwa mdogo.
Kutokana na hali hiyo, niliamua kufikiria kwa kina namna bora ya kutatua tatizo hili. Mwishowe, suluhisho limepatikana ambalo si tu linaweza kupunguza gesi ya CO₂, bali pia linaweza kuleta faida kiuchumi (fedha).
Suluhisho hilo ni kubadilisha gesi ya kaboni dayoksaidi kuwa mafuta ya petroli moja kwa moja ndani mtambo.
Katika mfumo wa mtambo, gesi ya kabon dayoksaidi (CO₂) iliyopo hewani na inayotoka kwenye magari kila siku itaweza kuvutwa na kukamatwa moja kwa moja kutoka angani kisha kuibadilisha kuwa mafuta ya petroli.
Kila siku, mfumo huu utakua ukiendelea kuzalisha mafuta na kuyahifadhi moja kwa moja. Mfumo huu pia una nozzle kwaajili ya kujaza mafuta kwenye magari.