Ujenzi wa mtambo wa kuchakata majitaka Mbezi Beach, uliopo Wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam, umefikia asilimia 80 na hivyo kuwa mbioni kukamilika. Mradi huo wa mfano na wa kipekee nchini unatekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa lengo la kuboresha huduma za usafi wa mazingira na kudhibiti athari za majitaka katika maeneo yanayohudumiwa.
Akizungumzia hatua ya utekelezaji wa mradi huo, Mhandisi Rahel Minja amesema maendeleo ya mradi yanaridhisha, huku kazi mbalimbali zikiwa katika hatua za mwisho kabla ya mtambo kuanza kufanya kazi na kutoa huduma kwa wananchi.
“Kwa sasa kazi kubwa ni kufunga vifaa na mitambo mbalimbali ya umeme, pamoja na kutengeneza mifumo ya majitaka na majisafi ili kukamilisha ujenzi wa mtambo huu. Ni matarajio yetu kuwa mradi utakamilika ifikapo Oktoba 30, 2026, na kuruhusu rasmi wananchi kuanza kuutumia,” amesema Mhandisi Rahel.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilongawima na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa, Issa Issa, amepongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo na kuwaasa wananchi kuwa tayari kuutumia na kuutunza mara utakapokamilika.
“Ni bahati kubwa mradi huu kuwa hapa kwetu. Hatuna sababu tena ya kuchafua mazingira kwa majitaka. Niwaombe sana wananchi watakaonufaika na mradi huu kuutunza vyema ili uweze kutusaidia kwa sasa na baadaye,” amesema Issa Issa.
Mradi wa Usafi wa Mazingira Mbezi Beach unajumuisha ujenzi wa vituo viwili vya kuchakata majitaka, mtandao wa mabomba ya majitaka wenye urefu wa kilomita 101, ujenzi wa chemba zaidi ya 2,000 pamoja na mtambo mkubwa wa kuchakata majitaka. Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kunufaisha zaidi ya kaya 11,000 katika kata za Kawe, Kunduchi, Wazo na Mbezi Juu, huku ukichangia kwa kiasi kikubwa kuboresha usafi wa mazingira na afya ya jamii katika maeneo hayo.