Mtambue father christmas (santa clause) ni nani

Mtambue father christmas (santa clause) ni nani

Kudo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2017
Posts
1,821
Reaction score
6,119
Watu wamekuwa wakijiuliza mara kadhaa huyu babu krismasi jina lingine Santa Claus ni mtu aliyekuwepo au ni hadithi za kufikirika tu kumuhusu?

Ni kweli Baba Krismasi(father christmas) alikuwepo.Santa Claus(father christmas) kama wengi tulivyozoea kumwita.jina lake nicholaus alizaliwa kati ya miaka ya 200 hivi ndani ya familia moja ya kitajiri huko Patara katika jimbo la Likia(lycia),Asia Ndogo.
alilelewa na kukua katika ukikristo tangu utotoni mwake. alipoteza wazazi wake alipokuwa bado kijana mdogo sana,na kurithi utajiri wa mali za familia yake.
Kuna simulizi kadhaa kumuhusu yeye jinsi alivyojitolea kuwasaidia watu wengi katika maisha yake kwa tabia yake ya huruma na upendo,moja ya kisa chake maarufu kuliko vyote ni hiki hapa:
kulikua na Mtu mmoja maskini sana ambaye alikuwa na mabinti watatu na alishindwa kuwalipia mahari kwa yeyote kati yao aolewa. Mtu huyo akapanga mpango wa kuuza mabinti zake kwa ajili ya shughuli za ukahaba,
Mtakatifu Nicholaus au (father Christmas) aliposikia mpango huo wa Baba kwa mabinti zake aliamua kuwasaidia japo kwa siri sana. Siku moja alikuja katika nyumba ya mtu huyo usiku na kurusha mfuko alioujaza dhahabu kupitia dirishani huku kukiwa na (fedha za kutosha kulipa mahari). usiku wa siku ya pili Father Chrismas alifanya hivyo hivyo mpaka siku ya tatu. lakini Usiku wa siku ya tatu mtu yule alimkamata father christmas, lakini Saint Nicholas(fatherchristmas) alimwomba asiseme neno lolote kwa mtu yeyote kuhusu suala hilo.
Tangu siku hiyo kitendo chochote cha wema cha aina hiyo kilimshuhudia, na watu walikuwa wakikihusisha na Mtakatifu Nicholas, Maarufu kama “father Krismasi” kutokana na desturi yake ya huruma kwa masikini na ugawaji wa zawadi kwa watoto kwa siri. Wengi walimchukuliwa kama mtu mtakatifu na Mtakatifu anayeishi.

Wakati Askofu wa Myra alipokufa, Mtakatifu Nicholas alichaguliwa kumrithi nafasi yake. mtakatifu Nicholas alipitia mateso kadhaa katika maisha yake alipelekwa uhamishoni kutoka huko Myra alipokuwa askofu na kufungwa na Mfalme Diocletian. Baadaye alikufa mnamo karne ya nne kati ya miaka 345 na 352 tarehe 6 Desemba, na alizikwa huko katika kanisa alilohudumu yake. Mwili wake tena baadaye tena ulichukuliwa na wafanyabiashara wa Italia mnamo mwaka 1087 na kuzikwa katika kanisa jipya huko Bari,Italia.

Alitajwa kama mtakatifu kutokana na fadhila zake za wema, Nikolasi alikuwa na sifa ya kutenda miujiza pamoja na uponyaji.
alikuwa na tabia ya kuwaletea watu maskini na watoto zawadi kwa siri; kwa hiyo anakumbukwa hadi leo kwenye sikukuu yake ambako watoto hupewa zawadi zinazowekwa ndani ya viatu au ndani ya soksi. Kutokana na desturi hii amekuwa pia kielelezo au chanzo cha Baba Krismasi(father christmas) ambayo ni desturi inayompambanua zaidi.

huko Ulaya karne za kati aliheshimiwa kama mtakatifu msimamizi wa mabaharia na wafanyabiashara;

Tarehe 6 Desemba wiki mbili kabla ya sikukuu ya krismasi kanisa huadhimisha siku yake inayosheherekewa na Wakristo Wakatoliki,na baadhi ya Waprotestanti Ulaya ya kati na kaskazini.

mji alipoteuliwa kuwa askofu kwa mara ya kwanza huko Myra leo hii unaitwa Demre, ni mji uliopo kusini mwa Uturuki, si mbali na Antalya.

Padri Martin Luther aliyewahi kujitenga na kanisa katoliki alitaka kusisitiza umuhimu zaidi wa Krismasi kwa Wakristo hivyo alitaka watu wakati huo kuacha desturi ya kuwazawadia watoto kwenye siku ya Mtakatifu Nikolasi tarehe 6 Desemba,huku akipendekeza kuhamisha zawadi kutoka kwa watoto hao kwenda kwa mtoto Yesu, adhimisho la siku ya kuzaliwa ili kumkumbuka zaidi Yesu kuliko mtakatifu huyo.akikumbushia zaidi zawadi zilizopelekwa kwa Yesu na mamajusi kutoka mashariki kama inavyoripotiwa katika Injili ya Mathayo2.Desturi ya kuwazawadia watoto kwenye sikukuu hii ilienea hadi kuwa desturi ya kupeana zawadi kati ya watu wa kila umri.
huyu ndiye mtakatifu nicholaus (father christmas)

KWANINI ANACHUKIWA SANA FATHER CHRISTMAS NA BAADHI YA MADHEHEBU
MIMI SIJUI ILA SOMA HAPA

WATOTO ulimwenguni pote wanampenda sana. Katika mwaka wa majuzi alipokea barua zipatazo 800,000 kupitia shirika la posta la Ufaransa, hasa kutoka kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka mitatu na minane. Inaonekana sanamu ya Baba Krismasi yenye ndevu nyingi nyeupe na joho jekundu lenye mapindo ya manyoya meupe, ni mojawapo ya vitu vinavyopendwa sana katika shamrashamra za sikukuu. Basi, je, unaweza kuwazia sanamu hiyo ikiteketezwa? Ndivyo ilivyotukia miaka 50 na kitu iliyopita huko Dijon, Ufaransa. Mnamo Desemba 23, 1951, Baba Krismasi “aliuawa” mbele ya watoto 250 hivi.

Alifanya kosa gani? Gazeti France-Soir lilisema kwamba aliteketezwa “baada ya makasisi kukubaliana kwamba alikuwa amenyakua cheo cha Kristo na alikuwa mwasi” na walimshutumu kwa “kufanya sherehe za Krismasi ziwe za kipagani.” Tangazo moja lilisema kwamba tendo hilo lilikuwa na maana fulani. “Uwongo hauwezi kuwafanya watoto wavutiwe na dini na si njia ya kuelimisha kamwe.”

Viongozi fulani wa dini walisema kuwa desturi zinazohusiana na Baba Krismasi zinawapotosha watu kutoka kwa “maana halisi ya Kikristo” ya kuzaliwa kwa Yesu. Na hata mtaalamu wa utamaduni, Claude Lévi-Strauss, alisema katika gazeti la Les Temps Modernes (Nyakati za Kisasa) kwamba imani ya Baba Krismasi ni “mojawapo ya mambo yanayofanya watu wengi wapende upagani leo.” Alisema pia kwamba dini ilikuwa na haki ya kuishutumu imani hiyo. Lévi-Strauss pia alionelea kuwa huenda imani ya Baba Krismasi ilianza zamani za kale wakati wa mfalme wa mungu-jua. Sikukuu ya mungu-jua ilisherehekewa katika Roma ya kale kuanzia Desemba 17 hadi 24. Wakati huo majengo yalipambwa kwa majani mabichi na watu walipeana zawadi. Sikukuu ya mungu-jua ilikuwa na shamrashamra kama za Krismasi.

Leo, zaidi ya miaka 50 tangu sanamu ya Baba Krismasi ilipoteketezwa, Wakatoliki nchini Ufaransa wana maoni gani kuhusu Baba Krismasi? Imani hiyo iliyoanza wakati wa sikukuu ya Roma ya Mungu-jua bado inatumiwa sana wakati wa Krismasi kama sanamu ya Yesu akiwa katika hori la ng’ombe. Pindi kwa pindi, makasisi hudai kwamba Baba Krismasi huwakilisha shughuli ya kibiashara ambayo huwafanya watu wamsahau Kristo wakati wa Krismasi. Hata hivyo, watu wanampenda sana Baba Krismasi hivi kwamba wamepuuza chanzo chake cha kipagani.

asalaam kudo
 
Correction!
Mkuu Kudo900 Martin Luther King hajawahi kulitenga Kanisa katorili bali RC Lilimtenga..!
 
Correction!
Mkuu Kudo900 Martin Luther King hajawahi kulitenga Kanisa katorili bali RC Lilimtenga..!
Chief upande huu upo good kiasi chake vipi kuhusu uhalali wa chrimas na uzao wa yesu a
Maana hadi sasa maandiko kadhaa yananichanganya kidogo kuhusu hiyo tarehe 25
But kuna makala naiandaa kuhusu hilo Hope na nyama zako zinaeza jazia pahali
 
Chief upande huu upo good kiasi chake vipi kuhusu uhalali wa chrimas na uzao wa yesu a
Maana hadi sasa maandiko kadhaa yananichanganya kidogo kuhusu hiyo tarehe 25
But kuna makala naiandaa kuhusu hilo Hope na nyama zako zinaeza jazia pahali
Andaa mkuu ngoja nami nianze kutafuta nondoz hizo za kuchangia kwa hiyo mada yako!
 
Chief upande huu upo good kiasi chake vipi kuhusu uhalali wa chrimas na uzao wa yesu a
Maana hadi sasa maandiko kadhaa yananichanganya kidogo kuhusu hiyo tarehe 25
But kuna makala naiandaa kuhusu hilo Hope na nyama zako zinaeza jazia pahali
usisahau kunitag
 
Back
Top Bottom