MTANANGE Simba V/S Coastal Union direct report

Status
Not open for further replies.
we shuleni mwalimu wako wa hesabu alipatata tabu kweli,

kwa kutumia elimu niliyonayo ngoja nijaribu kukufundisha,

mtu akikwambia 2 mara 3, ni sawa na mtu akikwambia 3 mara 2 umenielewa?

therefore, SIMBA VS COASTAL = COASTAL VS SIMBA.
mishabiki ya Yanga mengi kelele tu mbele giza,shabiki vitumbua kama Bantu lady
 
wadau tusitumie maneno makali sana .... najua hawa mayanga ni wagumu kuelewa ila tukitumia maneno makali hivyo yenye ukakasi tutaharibu. hawa ni wetu hawa.... sisi tuliwaletea shanga.kule kwetu ni kamba za kufungia ng'ombe. bantu lady amechooooooooooooooooooooooooooooooka. sijui yu wapi. makoye kaka upo?
 
We ndo hujui unachokisema ukisema simba vs coastal watu wataenda taifa lakin ukisema coastal vs simba wadau watajua ni mkwakwani Tanga. Hio ni tofaut na mahesabu yako

kwan mi nimetoa thread ya kuwaalika watu waende uwanjani?
 

sawa bwana mbumbumbu.
 
we shuleni mwalimu wako wa hesabu alipatata tabu kweli,

kwa kutumia elimu niliyonayo ngoja nijaribu kukufundisha,

mtu akikwambia 2 mara 3, ni sawa na mtu akikwambia 3 mara 2 umenielewa?

therefore, SIMBA VS COASTAL = COASTAL VS SIMBA.

Katika kuripoti soka ni tofauti mpwa....
Timu inayoanza kuandikwa hiyo ndiyo mwenyeji na inayofuata hiyo ni timu ngeni (visitors team).
Hivyo kwa mechi iliyoripotiwa hata ni lazima Coastal Union itaanza kuandikwa then Simba itafuatia.
Coastal U vs Simba SC.
 
Soka na masharobaro ni vitu viwili tofauti, umeacha kubana pua studio unakuja kuandika mambo ya uongo humu!
Mechi ya mwisho Simba alicheza na JKT Ruvu na sio Ruvu Shooting kama ulivyodanganya watu wazima.

Vile vile nahodha wa Yanga ni Nadir na sio Nadri, acha kukurupuka bwana mdogo.
 
mikia msipanic,mpira ukiisha kila mtu aongozane na mwenzake mpk hme mambo ya kuzimia na kulala huku mmesimama/kuipita nyumba yako kuingia ya jiran hatutak tena
 

Sijui yuko wapi aje amuone shabiki maandazi, shabiki fuata upepo wake. Hajitambui kabisaaa...
 
Mimi nadhani kuliko kuchangia uzi wa taahira kama hili lisilojielewa ni heri ukaanzishwa mwingine na mdau. Maana lengo la nyuzi kama hizi ni live update na kamwe sio kupotosha ukweli halafu hata pale mtu anapoelimishwa hataki kukubali ujinga wake.
Hapo ndipo ninapomkubali Makoye Matale kuwa ni mshabiki wa soka kweli. Mtu kama Makoye Matale kwenye ukweli anasimamia ukweli na kwenye makosa amekuwa akikubaki na hata kurekebisha taarifa za shabiki wa Yanga wenzake.

Lakini hawa wote wanaomsapoti huyu youngsharo hata nyuzi zao nyingi humu JF zinaonesha ni kwa kiasi gani ni wachanga wa soka na wakurupukaji tu.
 
Last edited by a moderator:
MZUNGUKO WA PILI LIGI KUU TANZANIA KAZI IPO NDANI YA MKWAKWANI SIMBA SC VS COASTAL UNION.
Wakati Simba SC imecheza mechi 12 huku ikishinda mechi 3 , droo 7 na kufungwa mechi 2 ipo nafasi ya 8 katika msimamo wa ligi na pointi 16 kibindoni wapinzani wao Coastal Union wao wamecheza mechi 13 huku wakishinda mechi 4 , droo 5 na kufungwa mechi 4 wapo nafasi ya 7 na pointi 17 .
Ukitazama uwiano kiufundi timu zote zinaonekana kushabihana.
Simba kadroo mechi 7 katika mechi 12 huku Coastal kadroo mechi 5 katika mechi 13, sasa 12-7= 5 wakati 13-5= 8 hapo utaona hakuna tofauti kabisa kwa sababu aliyecheza mechi nyingi ambaye ni coasta l anabebwa na droo ya mechi 5 huku Simba aliyecheza mechi chache anadroo 7 huku akishinda mechi 3 tu! Hapo utaona wote timu zao zinajilinda sana kuliko kushambulia ndio maana wana droo nyingi kuliko ushindi. Coastal kashinda mechi 4 Simba hiyo ndio inawapa tofauti ya pointi 1.
Timu zote zinategemea zaidi viungo wa kati na full backs kuanzisha mashambulizi hivyo utaona mpira mwingi unapigwa kati huku mashambulizi yakiwa ya kushitukiza au kutafuta zaidi ushindi kwa dead balls. Naweza sema Simba SC watakuwa na mtihani kidogo , sidhani kama backline ya Coastal itakubali kupoteza mechi 2 mfululizo. Game ya mwisho Wamefungwa 1-0 na YANGA.
DAKIKA 90 ZITAAMUA
All the best Mnyama mkali kuliko wote!! Wadau Freeland Makoye Matale, grafani11, Bantu lady, mkolaj, OKW BOBAN SUNZU daud Mchambuzi, Deo Corleone GENTAMYCINE MKALIKENYA, sembo KikulachoChako kbm Na wadau wote ambao nimesahau kuwataja hapa tunawategemea
 
Last edited by a moderator:
Mtu na mdogo wake hao! Sare inawafaa sana na inaendana na sera ya wakulima wa Bunju a.k.a wazee wa sare
 
Mkia leo sijui kama mtatoka salama...
 
Leo mnyama anamtafuna mtu uraiani na sio mbugani kama ilivyozoeleka.....wagosi wa kaya wajiandae kisaikolojia kukipokea kipigo cha kihistoria......MNYAMA SIMBA TU MBUGANI..........
 
Niko WAMI mungu akipenda baada ya masaa ma 3 naweza kua Tanga kwa ajili ya huu mtanange.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…