Mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya Simba Sports Club na Coastal Union ya jijini Tanga utakaofanyika hapo kesho umekuwa ni mchezo unaosubiriwa kwa hamu hasa kwa upande wa Simba,
ukizingatia kwamba mahasimu wao Dar_es Salaam Young Africa Sc Juzi Walifanya vizuri, hivyo hawana budi kukaza buti ili kuepukana na makelele ya mahasimu wao endapo watafungwa.
Simba ipo katika harakati za kujinasua dhidi ya kushuka daraja kwa kupoteza mwelekeo kwenye mzunguko wa kwanza, wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu nzuri ya mchezo uliopita baada ya kujinyakulia pointi 3 muhimu kutoka kwa Ruvu Shooting,
Aidha katika mechi ya juzi ya watani wao Yanga waliibuka na ushindi wa bao moja kwa mtungi dhidi ya hao Coastal Union goli lililofungwa na beki mahiri Nadri Haroub Al Maarufu (Canavaro) katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Hivyo Coastal Union hawatokuwa tayari kupoteza mechi mbili mfululizo nyumbani kwake.