Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Mbunge anayemaliza muda wake wa jimbo la Arusha mjini na aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa huo Mrisho Gambo @mrisho_gambo amechukua tena fomu ya kuwania nafasi ya kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi @ccmtanzania kuwa Mgombea wa Ubunge wa Jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania utakaofanyika baadae Mwaka huu.
Kitendo cha Gambo kuchukua Fomu hiyo kunafanya ushindani kuwa mkubwa baada ya Jana aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda kuchukua fomu na kutia nia ya kutaka kuwa Mgombea wa CCM katika jimbo hilo.
Maamuzi ya nani atapeperusha bendera ya Chama yatafanywa na Chama baadae na Kisha Mgombea atakayepitishwa atakuwa na kazi ya kuwashawishi Wananchi wampigie kura akawe mwakilishi wao kwenye Bunge lijalo la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.