Mtanange wa Klabu Bingwa Afrika: Al Ahly 5 vs Simba SC 0

Mpira wa tz .. ni wakwenye media ..kwenye performance huwa hamna kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika Usajili wa Klabu ya Simba sio wa Mashindano Makubwa kama haya ya Klabu Bingwa Afrika.Kama kweli Mwekezaji wa Klabu ya Simba Mohamed Dewji anataka Klabu yake ifanye vizuri basi sio kwa Wachezaji hawa.Kwa walioangalia mchezo wa Simba na Al hary atakubaliana nami kuwa Safu ya ulinzi wa timu hiyo ni mbovu kabisa .Wachezaji hawa kwa uwezo wao ni kwa Local Matches za ndani kwa maana ya Ligi Kuu , uwezo wao ni wa kucheza na Yanga, Ndanda na Stend United.Naushauri Uongozi wa Simba ifanye mabadiliko makubwa kwa wachezaji wake itafute wachezaji wenye uzoevu mkubwa na pia Kocha mkuu nae naona uwezo wake umefika mwisho.Mwisho namshauri Mtaani wetu kwa kuwa mwaka 2019 yeye ndio Bingwa basi ajipange vilivyo kwani wachezaji kama Boban Fey Toto hamna kitu kwa Mashindano haya ni magumu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba ikiongozwa na ushabiki ujinga wa yule mzungu.
Nafikiri sasa ni wakati muhimu atulie na atimize majukumu yake ya habari na sio kipiga domo.
 
sema aishi manura bado ana khali ya kimchezo naona anaokota mpira haraka haraka akiamini watarudisha hahahaha kumbe anawahisha kipigo
 
Simba ina foreigners wangapi walioanza mechi hii? Ukisema mpira wa bongo bado sana maana yake hata hao wageni wanachezea simba ni watz ambao uwezo wao upo chini sana[emoji39][emoji39][emoji39]
Poleni wana simba, poleni Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…