carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Said Mtanda, ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani humo kuwasaka, kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu wanaodaiwa kuiba betri 40 za mashine ya CT Scan na swichi ya kubadili umeme katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.
Mtanda ametoa agizo hilo jana, tarehe 19 Oktoba 2026,baada ya kufanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo na kubaini wizi wa vifaa hivyo, ambavyo serikali imewekeza fedha nyingi kuvinunua kwa ajili ya kuboresha huduma za afya.
Amesisitiza kuwa wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo wanapaswa kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria mara moja.
Wizi huo unazua maswali kuhusu usalama wa vifaa vya hospitalini vilivyonunuliwa kwa fedha za umma na umuhimu wa kuwepo kwa mifumo madhubuti ya kulinda mali za serikali.
Katika ziara hiyo, Mtanda pia amewataka watumishi wa hospitali hiyo kutanguliza maslahi ya wananchi kwa kuzingatia maadili, uadilifu na misingi ya taaluma zao.
Amesema Serikali ina matarajio makubwa kwa watumishi wa afya katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, hivyo wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa uwajibikaji na kulinda vifaa vinavyotumika kutoa huduma hizo.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Dk.Athanas Ngambakubi amesema wamesharipoti polisi na wanaendelea kuchunguza wizi huo.
Ngambakubi amesema taarifa za awali zilionyesha betri hizo zilikuwa zikichukuliwa kwa awamu huku baadhi ya watu waliohusika na usafirishaji wakitajwa kuwa na taarifa zinazoweza kusaidia kupata uchunguzi.
Amesema dereva bodaboda aliyekuwa akibeba betri hizo alitoa ushirikiano na polisi wameshapata mwelekeo kuhusu mahali zilipo betri 16 kati ya 40.
Chanzo : Mwana halisi