Mtandao Mkubwa Waliotengeneza Lowassa na Kikwete Katika Siasa ya Tanzania

Mtandao Mkubwa Waliotengeneza Lowassa na Kikwete Katika Siasa ya Tanzania

Mtanzania2020

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2020
Posts
1,033
Reaction score
2,307
Kitu ambacho tumejifunza katika siasa za hapa Nyumbani ni kwanba Mzee Lowasa na Mzee Jakaya hawataacha kujitokeza katika Makundi ya Siasa zetu.

Na kama kuna kitu walifanikiwa katika hili Taifa Basi walijenga mfumo wao kwa akili na maarifa katika Kujenga mtandao ndani ya Siasa za Taifa Letu.

Hawakutengeneza vijana Machawa bali vijana wavumilivu, watu wa mikakati, watulivu na wenye sifa za kupewa nafasi yoyote kwa mtawala yoyote.

Na Sifa kubwa ya hawa Wazee hawakuwa wachoyo kabisa walitengeneza vijana matajiri ambao huwatishi kuna wakati JPM alikutana nao akawa anajaribu kuwapiga panga ila kadri alivyokuwa anawapiga mapanga ndio walikuwa wanamsogelea zaidi.

Hawa wazee walijenga mtandao fungamanishi yaani Chamani wamo, serikalini wamo.

Itachukua miaka kadhaa kufuta kabisa huo mtandao wa hawa hawa wazee, na kiongozi wa hili Taifa yoyote usalama wake mkubwa utategemeana na Mtandao wa hawa wazee amewapunguza kiasi gani au umeushirikisha kiasi gani.

#NondozaSiasa
FB_IMG_1753258637429.jpg
 
Mwanamtandao sikiliza, Hao wahuni Hawana pawa yoyote watanzania bado ujinga ni mwingi hawajaamua kuwanyoosha.....na hao wanamtandao wenyewe njaa zinawasumbua tu wametanguliza matumbo mbele.
 
Ukarabati wa mfumo au system overhaul ndio muarobaini.
Tutakapofanya ukarabati tutanyofoa na kutupilia mbali ambavyo havitufai.
Madai ya reform ni mkakati madhubuti wa kuondoa uozo na kujenga mfumo imara na thabiti.
 
Back
Top Bottom