Mtandao, mtandao, mtandao. Je tumekabidhi maisha yetu kwa mtandao?

Mtandao, mtandao, mtandao. Je tumekabidhi maisha yetu kwa mtandao?

herzegovina

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2015
Posts
3,155
Reaction score
4,744
1. Mshkaji wako amekukopesha pesa umrudishie baada ya wiki moja. Anakusisitizia kuwa hakikisha unamlipa kwa wakati kwa kuwa anataka kupeleka mtoto shule. Siku inafika, bahati mbaya unakuwa kwenye kikao kizito ofisini kwenu kinachochukua muda mrefu sana mpaka simu yako inazima. Jamaa kila akipiga anaona hupatikani. Unachelewa mno kutoka job unawahi home kuchaji simu lakini hakuna wakala aliye wazi. Unakutana na sms za mshkaji kuwa alikutafuta mara 14. Unaona ni usiku sana, hivyo humjibu chochote ukiamini asubuhi utamtumia pesa yake. Asubuhi anakupigia unawahi kupokea na kumwambia, "sasa hivi mwanangu, nakutumia". Unakwenda kwa wakala unamwambia unataka kutuma pesa kwenda mtandao fulani, anakujibu "mtandao unasumbua BRO".

2. Umecheza mkeka wako safi, umetiki TSH 387,000/=. Kesho yake unaamka huna pesa hata mia ila una mkeka uliotiki tu na una hamu ya bata, unawashtua washakaji zako wawili mnakaa sehemu mnapata supu kisha mnaendelea na bia mbili tatu. Unawaambia washkaji waendelee na unachukua bodaboda akupeleke kwenye BET SHOP uka-payout mkeka wako kisha akurudishe. Unakuta watu wamekaa pembeni na KAUNTA zipo tupu kabisa. unasogelea KAUNTA unamuona mdada wa ndani anachat tu. unamwambia dada naomba unilipe mkeka wangu, anakujibu "leo mtandao hakuna"

3. Unawawaita Mafundi "site" kwako wahakikishe wanachimba msingi na kupandisha mjengo hadi kwenye "LENTA" na kazi isilale. Unawaacha site unakwenda kwenye mihangaiko yako. Saa nane inafika, unaingia benki ukachukue pesa za mafundi unakuta foleni kali sana. unakwenda nayo weee mpaka unakuwa mtu wa tano kutoka mbele. Ghafla unaona huduma imekata kwani aliyekwenda dirishani anarudi tena kwenye mstari. Unamuuliza vipi, anakujibu "mtandao umekata"

4. Umekwenda Manispaa kulipia ada ya kiwanja chako, baada ya foleni ndefu sana unafika mbele kabisa, unaambiwa "mtandao unasumbua"

5. Mkeo anaugua kwenye "tarehe dume" (zile tarehe ambazo unajidai unapenda sana dagaa lililochanganywa na bamia na nyanya chungu) bahati nzuri una bima ya afya. Unakwenda hospitali anapata "mavipimo" kibao kisha anaandikiwa dawa lukuki tena za bei ghali sana ambazo anatakiwa aanze immediately. Unakwenda dirishani hospitali unaambiwa hizo dawa hazipo. Unatoka kutafuta duka la dawa linalopokea bima ya afya unalipata. Mfamasia anaanza kuzitafuta dawa kisha anakwambia "hayaa...hebu rudi hospitali kamwambie yule mfamasia aipost kwanza hii". Unarudi hospitali ili mfamasia aipost anakwambia "subiri kidogo bro, mtandao unasumbua"

HAKUNA DAWA YA HII KITU?
 
Back
Top Bottom