GE2025 Mtandao wa Bloga Tanzania yawaonya wanaotabiri majanga, "wanaleta taharuki"

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mtandao wa Bloga Tanzania (TBN) umekemea vikali tabia inayoshamiri ya watu kujinadi kufanya utabiri kwa watu na taifa kupitia mitandao ya kijamii, ukisema vitendo hivyo vinakiuka Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Kauli hiyo imetolewa kama azimio katika kikao kazi cha mafunzo ya mabloga kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Mabloga hao wameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) kushirikiana kuwasaka na kuwachukulia hatua kali wale wote wanaohusika na vitendo hivyo.

Katika kikao hicho, mabloga walibainisha kuwa kumeibuka kundi la watu wanaodai kuwa ni manabii na kutoa kauli zinazokiuka sheria za nchi na kuleta taharuki kuelekea uchaguzi.

Walisisitiza kuwa baada ya kuchambua Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (Personal Data Protection Act), walibaini kwamba ‘utabiri’ wa namna hiyo unavuruga haki ya msingi ya faragha ya wahusika.

Kwa mujibu wa Bw. Innocent Mungy, mtoa mada kutoka Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), sheria hiyo inakataza mtu kuzungumziwa kuhusu afya yake, mwenendo, au taarifa zake binafsi kutolewa bila ridhaa yake. Mungy alisisitiza kuwa sheria hii ina adhabu kali na lazima ifuatwe na kila mtu, si tu mabloga na waandishi wa habari.

Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na TCRA, yalilenga kuwaandaa mabloga kuripoti habari za uchaguzi kwa weledi na uadilifu.

Screenshot 2025-08-12 011507.png
 
Mtandao wa Bloga Tanzania (TBN) umekemea vikali tabia inayoendelea kushamiri ya watu kujinadi kufanya utabiri kwa watu binafsi na baadhi ya viongozi kupitia mitandao ya kijamii, ukieleza kuwa vitendo hivyo vinakiuka Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Kauli hiyo imetolewa leo August 11, 2025, jijini Dar es Salaam katika kikao kazi cha mafunzo ya mabloga kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, ambapo washiriki walikubaliana kuchukua msimamo wa pamoja kulinda maadili na weledi wa mawasiliano mtandaoni.

Mabloga hao wamezitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) kushirikiana kuwasaka na kuwachukulia hatua kali wote wanaojihusisha na vitendo hivyo, wakisisitiza umuhimu wa kutekeleza sheria bila upendeleo.

View attachment 3438748
Hahaha yaani ukweli ukisemwa watu instead of kuchukua hatua wanaongea ujinga, mjiangalie ...
Shauri yenu
 
Mtandao wa Bloga Tanzania (TBN) umekemea vikali tabia inayoendelea kushamiri ya watu kujinadi kufanya utabiri kwa watu binafsi na baadhi ya viongozi kupitia mitandao ya kijamii, ukieleza kuwa vitendo hivyo vinakiuka Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Kauli hiyo imetolewa leo August 11, 2025, jijini Dar es Salaam katika kikao kazi cha mafunzo ya mabloga kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, ambapo washiriki walikubaliana kuchukua msimamo wa pamoja kulinda maadili na weledi wa mawasiliano mtandaoni.

Mabloga hao wamezitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) kushirikiana kuwasaka na kuwachukulia hatua kali wote wanaojihusisha na vitendo hivyo, wakisisitiza umuhimu wa kutekeleza sheria bila upendeleo.

View attachment 3438748
Kwa kweli waache kuzua taharuki
 
Ukiwatazama tu hao Wajumbe unagundua mpaka Oktoba nusu yao watakuwa Wamekufa.
 
Back
Top Bottom