Mtandao wa chanjo ya Corona ya Pfizer na BioNTech wadukuliwa

Mtandao wa chanjo ya Corona ya Pfizer na BioNTech wadukuliwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Kumetokea shambulizi la kimtandao ambalo limezilenga data za makampuni yaliovumbua chanjo ya virusi vya corona, Pfizer na BioNtech, likiwa ni sehemu ya uhalifu wa kimtandao ambao unayoyalenga Makampuni ya Dawa ya Ulaya (EMA) huko mjini Amsterdam, Uholanzi.

Taarifa hiyo imetolewa kwa pamoja na makampuni hayo baada ya pia kuwasilisha taarifa yao kwa asasi ya ulezi ya makampuni hayo EMA.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo baadhi ya nyaraka zake zenye kuhusika na udhibiti wa chanjo ya Pfzer na BioNTech ambazo zimehifadhiwa katika kumbukumbu za EMA zimeingiliwa kinyume cha sheria.

Msemaji wa EMA amesema shirika hilo linachukua hatua za kisheria. Chanjo ya makampuni hayo ndio iliyoonesha uwezo wa kinga kwa asilimia 95, miongoni mwa watu 30,000 ambao walifanyiwa majaribio.
 
Back
Top Bottom