Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMENT) pamoja na Kituo cha Sheria na haki za binadamu LHRC wameendelea kuisisitiza Serikali kuhusiana na kufutwa kwa adhabu ya viboko shuleni badala yake kubuniwe kwa adhabu ngingine zenye kuongeza stadi za maisha kwa mwanafunzi.
Msisitizo huo umekuja hivi karibuni baada ya kuripotiwa kifo cha mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya sekondari Mwasamba mkoani Simiyu ambacho kinatajwa kimetokana na adhabu ya viboko iliyotolewa na Mwalimu wake.
Mratibu wa TENMENT Kitaifa Martha Makala amesema watu wengi wanafikiri kutokana na mazingira yalivyo katika shule zetu ni vingumu kuondoa adhabu ya viboko ingawa kwenye maboresho ya sheria ya elimu kunasisitizwa kuondolewa kwa mustakabali wa ulinzi na usalama wa mwanafunzi.
Shida sio viboko bali utaratibu wa adhabu za viboko umekaaje.
Mtoto ana adhibiwa kwa viboko kwa idadi maalumu mfano fimbo 5 au 10 kwa kosa na mzazi anatakiwa kutaarifiwa na yeye ashiriki adhabu sababu watoto hawajaanza kuwa wakaidi miaka hii ila ni wazazi wameanza kuwaachia walimu watoto wakaidi wawanyooshe pekee yao.
Tunapopigia chapuo kitu tuangalie na lengo kuu ni nini nyuma ya maandamano au kukemea.
Unasema watoto wasichapwe nini mbadala wake wapigwe masingi au wazomewe?
Nadhani kwasasa magepu yaliyopo ni walimu tunaowaachia watoto saikolojia yao ipoje?
Isije ikawa wanapiga watoto badala ya kuwaadhibu.
Je,wanatoa adhabu kwa kiwango kipi? Maana mwalimu anashika fimbo kwanza hajui kuwa fimbo ina size maalumu,kuna fimbo ya kuchapia mwizi na ya kuchapia mtoto mkaidi. Fimbo kubwa halafu anapokwenda kutoa adhabu kifuani ana hasira debe zima ambazo hazihusiani na huyo mwanafunzi,na anapoanza kumuadhibu lengo linakuwa ni kumpiga na sio kumuadhibu kwa viboko ambavyo idadi yake itategemea na yeye mkono wake ukishachoka.
Na unaweza shangaa baada ya kuchoka mwingine anasema hebu nipe na mimi nimuonje kidogo, anaendelea kupiga wanasahau kuwa yule ni mwanafunzi na adhabu ni kwaajiri ya kumrekebisha sio kumkomoa plus wanatakiwa kucheza na akili ya mwanafunzi yenye ukaidi na sio kudeal na matokeo ya ukaidi wake.
Binafsi naona tatizo la msingi sio viboko kwani vimekuwepo kwa miaka mingi, ILA tatizo kubwa
ni ukosefu wa ajira uliopelekea baadhi ya watu wasiokuwa na mapenzi na kazi ya Ualimu kuingia kwenye fani kwa ajili ya kupata ajira. Ni sawa tu na tunavyo pata changamoto ya baadhi ya manesi kutumia lugha isiyo nzuri kwa kina mama, ila ukichunguza kwa makini utagundua ni tatizo la ajira lililopelelea watu wasio stahili kuingia kwenye fani hiyo.....
uko sawa kiongozi. mimi madogo wakiharibu natandika viboko ila sio vile vya kupiga hovyohovyo. kwanza lazima namweleza kosa lake na alitambue na adhabu yake inatamkwa hapohapo. kama ni viboko dogo atachapwa viboko idadi maalum niliyokwishamtamkia.