Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMENT) pamoja na Kituo cha Sheria na haki za binadamu LHRC wameendelea kuisisitiza Serikali kuhusiana na kufutwa kwa adhabu ya viboko shuleni badala yake kubuniwe kwa adhabu ngingine zenye kuongeza stadi za maisha kwa mwanafunzi.
Soma: Simiyu: Mwanafunzi adaiwa kufariki kwa kuchapwa viboko na kukanyagwa kichwani na mwalimu shuleni
Msisitizo huo umekuja hivi karibuni baada ya kuripotiwa kifo cha mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya sekondari Mwasamba mkoani Simiyu ambacho kinatajwa kimetokana na adhabu ya viboko iliyotolewa na Mwalimu wake.
Mratibu wa TENMENT Kitaifa Martha Makala amesema watu wengi wanafikiri kutokana na mazingira yalivyo katika shule zetu ni vingumu kuondoa adhabu ya viboko ingawa kwenye maboresho ya sheria ya elimu kunasisitizwa kuondolewa kwa mustakabali wa ulinzi na usalama wa mwanafunzi.