JamiiCheck
JF-Expert Member
- Nov 3, 2023
- 245
- 267
Kipindi cha Januari hadi Juni 2025 kimeonesha ongezeko kubwa la taarifa potofu, hususan zinazohusiana na siasa. Katika muda huu, JamiiCheck ilihakiki jumla ya madai 192, ambapo madai ya yasiyo ya Kweli yaliongoza kwa kuwa 128 sawa na asilimia 67 ya madai yote. Madai ya kupotosha yalifikia 42 (asilimia 22), wakati madai ya kweli yalikuwa 19 (asilimia 10) na nadharia zilikua tatu pekee (asilimia 1).
Masuala ya uchaguzi yalitawala kwa kiasi kikubwa, yakichangia madai 121 ambayo ni asilimia 63 ya madai yote yaliyohakikiwa. Kwenye kundi hili, vyama vya upinzani vililengwa zaidi kwa madai 101 (asilimia 53), vikifuatiwa na viongozi wa dini waliokuwa na madai 15 (asilimia 8). Rais Samia alihusishwa na madai matatu pekee (asilimia 2), huku CCM ikihusishwa na madai manne (asilimia 2). Madai mengine ya kijamii yalikuwa 69 (asilimia 35).
Kuhusu mbinu za upotoshaji, kuiga taswira (visual impersonation) kupitia zana rahisi kama Canva na Adobe kuliibuka kama mbinu kuu, na kuhusiana na asilimia 64 ya taarifa zote. Zaidi ya hapo, asilimia 32 ya maudhui yalikuwa ni ya kweli lakini yaliwekwa kwenye muktadha wa uongo, huku asilimia 4 pekee yakitokana na teknolojia ya AI, ikiwemo deepfakes. Ingawa kiwango cha matumizi ya AI bado ni kidogo, kimekuwa kikiongezeka kila mwezi, ishara ya hatari kubwa siku zijazo.
Kwa upande wa vyanzo, Facebook iliibuka kama chanzo kikuu cha taarifa potofu, ikiwa na madai 94 (asilimia 49) kutokana na upatikanaji mpana wa jukwaa hilo nchini. X (zamani Twitter) ilichangia madai 68 (asilimia 35), huku WhatsApp ikihusiana na madai 12 (asilimia 6). Mitandao mingine kama Instagram, Telegram, TikTok pamoja na tovuti mbalimbali ilihusiana na madai 18 (asilimia 10).