KERO Mtandao wa Halotel Tanzania umedorora kwa kiwango cha kushangaza, ukionyesha udhaifu mkubwa katika utoaji wa huduma za mawasiliano

KERO Mtandao wa Halotel Tanzania umedorora kwa kiwango cha kushangaza, ukionyesha udhaifu mkubwa katika utoaji wa huduma za mawasiliano

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Davidmmarista

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2024
Posts
1,367
Reaction score
2,451
Katika siku za hivi karibuni, wateja wamekuwa wakijiunga na kifurushi cha GB 10 cha mwezi mzima, lakini ndani ya siku tatu tu, bando limekwisha, huku matumizi halisi ya data yakionyesha kiwango cha 1GB kwa kila siku tatu. Huu ni ushahidi wa wazi wa kasoro katika mfumo wa usimamizi wa data au hujuma dhidi ya watumiaji.

Zaidi ya hayo, mtandao umekuwa haupatikani kwa muda mrefu, jambo ambalo si tu linakwamisha mawasiliano bali pia linadhoofisha uchumi wa wateja wenu wanaotegemea huduma za intaneti kwa shughuli zao za kila siku.

Kama kampuni haiwezi kutoa huduma bora kwa wateja wake, basi hakuna sababu ya kuendelea kuwepo sokoni. Ni heri kubaki na kampuni chache lakini zenye huduma za uhakika kuliko kuwa na kampuni zinazoleta kero na hasara kwa watumiaji wake.

Ni wakati wa Halotel kuwajibika ama kupisha nafasi kwa watoa huduma wenye uwezo wa kweli wa kuheshimu na kuhudumia wateja wao ip
asavyo.
 
Mbona mimi hizo ghasia sizipati, tokea nianze kutumia simu mtandao wangu ni halotel na siwezi kubadilisha.
GB 10 ni wiki ya 3 sasa natamba nayo.
Kwa nyie mnaotumia kwa kujifurahisha sio mbaya, ila kwa watu wa kazi huo mtandao haufai kabisa ,unadownload na kufungua siku nzima yaani uko slow sana,na unapotea mara kwa mara
 
Kwa nyie mnaotumia kwa kujifurahisha sio mbaya, ila kwa watu wa kazi huo mtandao haufai kabisa ,unadownload na kufungua siku nzima yaani uko slow sana,na unapotea mara kwa mara
fungua 4G uone spidi mbili zakutafuna mb na kasi...🤣
 
Back
Top Bottom