KERO Mtandao wa Halotel Tanzania umedorora kwa kiwango cha kushangaza, ukionyesha udhaifu mkubwa katika utoaji wa huduma za mawasiliano

KERO Mtandao wa Halotel Tanzania umedorora kwa kiwango cha kushangaza, ukionyesha udhaifu mkubwa katika utoaji wa huduma za mawasiliano

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hawa si ndio mtu unapiga simu haijaita imepokelewa na hamna mazungumzo mpaka urudie kama mara tatu ndio simu iweze kuita kwa hali ya kawaida.
 
Nimeanza kutumia simu 2017😂 nilipomaliza form 4
anhaaa kumbe sio mdogo sana upo kati ya 2000 mpaka 2003.

Ila kusema umeanza ulipomaliza form 4 ni kamba hiyo, sema ile rasmi ndio hiyo ila kiwiziwizi ni tangu primary.

Ishu ya simu imenifarakanisha sana na dogo langu la kike aisee, ni wasumbufu sana ninyi vitoto vya buku mbili dadeki zenu.
 
Wana gharama nafuu za bando zao , ila hizo bando zinakuwa ni feki yaani unaambiwa umepokea GB10 kwa 10k ila actually ni GB4 kwa 10k ,
 
Katika siku za hivi karibuni, wateja wamekuwa wakijiunga na kifurushi cha GB 10 cha mwezi mzima, lakini ndani ya siku tatu tu, bando limekwisha, huku matumizi halisi ya data yakionyesha kiwango cha 1GB kwa kila siku tatu. Huu ni ushahidi wa wazi wa kasoro katika mfumo wa usimamizi wa data au hujuma dhidi ya watumiaji.

Zaidi ya hayo, mtandao umekuwa haupatikani kwa muda mrefu, jambo ambalo si tu linakwamisha mawasiliano bali pia linadhoofisha uchumi wa wateja wenu wanaotegemea huduma za intaneti kwa shughuli zao za kila siku.

Kama kampuni haiwezi kutoa huduma bora kwa wateja wake, basi hakuna sababu ya kuendelea kuwepo sokoni. Ni heri kubaki na kampuni chache lakini zenye huduma za uhakika kuliko kuwa na kampuni zinazoleta kero na hasara kwa watumiaji wake.

Ni wakati wa Halotel kuwajibika ama kupisha nafasi kwa watoa huduma wenye uwezo wa kweli wa kuheshimu na kuhudumia wateja wao ip
asavyo.
Sitoshangaa kuona umeuzwa kama ZANTEL
 
Back
Top Bottom