DOKEZO Mtandao wa kifamilia ulivyoteka sekta ya uingizaji wa magari Japan - Tanzania

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Katika hali inayoashiria mtandao wa fedha haramu, familia moja yenye uhusiano wa karibu na vigogo nchini Tanzania inadaiwa kuteka mfumo mzima wa uagizaji wa magari ya mtumba kutoka Japan, na kuelekeza mabilioni ya fedha za Serikali katika mifuko yao, huku kukiwa na mgongano mkubwa wa kimaslahi.

Katikati ya mtandao huu yupo mfanyabiashara anayejulikana kwa jina la Prosper Sugai, au Japheth Benedict Nguku. Mtanzania aliyepata uraia wa Japani, na mmiliki wa kampuni ya ukaguzi wa magari iitwayo EAA Company Limited.

Kampuni hii inatajwa kuwa kitovu cha mtandao unaodhibiti kila hatua ya safari ya gari kutoka mnada wa Japani hadi barabarani Tanzania, huku ikihakikisha hakuna mkaguzi huru anayeweza kubaini dosari muhimu.

Mtandao wa Familia

Uchunguzi umebaini muundo ulio wazi, ambapo Mkaguzi yaani kampuni ya EAA Company Ltd (ya Prosper Sugai) ndiye wakala rasmi wa ukaguzi wa magari yanayopelekwa Tanzania (Pre-Shipment Verification of Conformity- PVOC) nchini Japan.

Waagizaji ni pamoja na kampuni mbalimbali zinazomilikiwa na familia yake wa karibu, akiwamo Rosper International (mpwa Thomas Brown), Real Motors International (kaka Josiah Nguku), Yune International (kaka Yune Nguku) na Be Forward Tanzania, inayohusishwa na mpwa Daniel Mtaalam.

Katika usafirishaji, ipo kampuni ya Prime Consolidators (kaka Kevin Nguku) kwa ajili ya upakiaji, Afritel (kaka Josiah Nguku) kwa ushughikiaji wa mizigo na upitishaji forodha Tanzania.

Upitishaji wa Fedha: ipo kampuni ya Omros, yenye utata inayoendeshwa na mshirika wa karibu wa Sugai. Vyanzo vinaeleza kuwa Omros ndicho kituo kikuu cha utoaji rushwa, chenye mitandao Yokohama (Japani), Afrika Kusini, maeneo ya Caribbean, na muhimu zaidi—Miami, Marekani. Mtandao huu hufanikisha usafirishaji na kuficha faida za mtandao huu wa kifisadi duniani kote.

Mtandao huo unajenga pisha ya mgongano wa kimasilahi kwamba, inawezekanaje EAA kuikagua kwa uadilifu mizigo ya magari inayotumwa na kampuni za ndugu zao ambao wanapata faida tu kama magari yatapita ukaguzi?

Kimsingi mumo huo umetengenezwa kwa ajili ya kupitisha magari kwa muhuri wa kirafiki, bila kuzingatia ubora.

7b59c664-7a94-42c9-8ca0-a7517d90368d.jpg

Rais Magufuli alishtukia mchezo

Machi 2021, hayati Rais John Magufuli, kwa misingi ya utaifa, alifuta mfumo wa PVOC ambao asilimia 70 ya ada zilikwenda kwa mawakala wa kigeni kama EAA. Akaanzisha Destination Inspection (DI), ambapo TBS wangefanya ukaguzi bandari ya Dar es Salaam.

Matokeo yalikuwa ya haraka na ya kuvutia: ndani ya miezi sita, TBS ilikusanya Sh bilioni 3.9, fedha ambazo hapo awali zingewafaidisha mawakala binafsi. Serikali ilikuwa imerejesha haki yake.

Ni wazi kwamba sera ya DI ilikuwa tishio la uhai wa biashara za kina Prosper Sugai na EAA, kwani iliifuta kabisa biashara yao ya mabilioni ndani ya siku moja.

Baada ya Magufuli kufariki, mrithi wake, Rais Samia Suluhu Hassan, alitoa maagizo kwamba magari yakaguliwe kule yanapotoka akidai kuwa utaratibu wa kuyakagua yanapofika nchini una urasimu.

Inadaiwa kuwa mpaka agizohilo linatoka, kulikuwa na ushawishi wa kampuni za ukaguzi wa magari zikitumia vigogo wa Serikali.

Inadaiwa kuwa Balozi Hussein Kattanga, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Japani (2020–2021), alihusishwa.

Taarifa Zaidi zinaeleza kuwa hatua muhimu zaidi ilikuwa kumhusisha Abdul Halim Hafidh, mtoto wa mtu mashuhuri sana ndani ya Familia ya Rais. Hafidh alifungua ofisi kamili Yokohama, Japan, na kuwa kitovu muhimu cha mtandao huu.

Kwa ushirikiano huu wenye nguvu, mabadiliko yalikuwa ya haraka.
Machi 2022, serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ilirejesha mfumo wa PVOC, kwa madai kuwa Tanzania “haina ujuzi wa kutosha,” kinyume kabisa na rekodi ya mafanikio makubwa ya TBS miezi michache tu kabla.

Vyanzo vinaeleza kuwa EAA hutenga USD 50 kwa kila gari kama malipo ya kufanikisha mfumo haramu wa mwamala. Kwa Tanzania kuagiza takribani magari 70,000 kila mwaka, hii ni USD milioni 3.5 (zaidi ya Sh bilioni 8.5) kila mwaka. Kwa mkataba wa miaka minne, mtiririko wa fedha unaofujwa unakaribia Sh bilioni 34.

Baada ya kufanikisha dili hilo, inadaiwa kuwa Balozi Kattanga, alirudishwa Tanzania na kuteuliwa Katibu Mkuu Kiongozi. Mwaka 2023 akawa Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Washington D.C na kisha mwaka 2025, EAA ikafungua ofisi mpya ya ukaguzi Miami, Marekani, ishara kuwa mtandao unazidi kupanuka kimataifa.

Madhara yake

Familia ya Sugai-Nguku, kupitia kampuni zao zilizounganishwa, inadhibiti, Kiwango cha ubora (kupitia mamlaka ya ukaguzi ya EAA), uagizaji (kupitia kampuni zao nyingi za kuagiza magari) na usafirishaji na Forodha (kupitia kampuni za ndugu zao).

Matokeo yake ni upotrevu wa fedha za Serikali, ushindani wa kibiashara umedhoofishwa na wananchi wanaishia kununua magari yasiyokaguliwa kwa usalama bali kwa faida ya mtandao huu.
 
Yaani watanzania akina TBS ndio wakague magari!!!,
PAmoja na kumpenda Jiwe ila kwenye hili ninapinga!
Ni bora yakaguliwe hukohuko Japan, TBS wana urasimu sana wanatengeneza mazingira ya kutaka rushwa hata kama gari halina shida
 
Sasa hivi Magufuli anakumbukwa na mengi
 
Detailed information, umepiga kwenye mshono🙏
 
Anyway, wakati TBS wamepewa kazi hio ilikuwa nzuri kimapato lwa serikali ila kwa mteja(mwananchi) hali ilikuwa mbaya sana. Usumbufu wa kijinga sana ulianzishwa ili mradi tu utoe rushwa na ilibidi maana gari ishafika inakula storage tu kwa urasimuvwa hawa watu wa TBS. Lengo lilikuwa zuri ila utekwlezaji wa TBS ilikuwa kichomi.
Cha piki JP kuna kampuni nyingi za kuagiza magari sio lazima utumie kampuni hizo nne au tano za hao watu.
 
Yaani watanzania akina TBS ndio wakague magari!!!,
PAmoja na kumpenda Jiwe ila kwenye hili ninapinga!
Ilileta shida shida sana, iliporudishwa JP watubwengi tulishukuru. Nia nzuri kwapa waTz kazi ila waTz wenyewe watu wa hovyo.
 
Anyway, wakati TBS wamepewa kazi hio ilikuwa nzuri kimapato lwa serikali ila kwa mteja(mwananchi) hali ilikuwa mbaya sana. Usumbufu wa kijinga sana ulianzishwa ili mradi tu utoe rushwa na ilibidi maana gari ishafika inakula storage tu kwa urasimuvwa hawa watu wa TBS. Lengo lilikuwa zuri ila utekwlezaji wa TBS ilikuwa kichomi.
Cha piki JP kuna kampuni nyingi za kuagiza magari sio lazima utumie kampuni hizo nne au tano za hao watu.
Umemaliza kilakitu 🫡
 
Naikumbuk hii issue gar zilikaguliwa baada ya muda waksema zikaguliwe huko huko …Kama nch ina mipigo mingi sana kila sector ni upigaji tuu no way out mifumo yetu na watu ni corrupt sana
 
Mkiambiwa mama yenu ni mtu wa ajabu mnakwa wabishi sana, haya ngoja tuendelee kulisakata lumba.
 
Mkuu mada nzuri sana, ila hujasema unashauri nini kifanyike, yaani conclusion ni nini? Urudi utaratibu wa JPM? Mtandao wa Familia upunguziwe majukumu? Au?
Na je mfumo mpya umesababisha kusiwe na fair competition kwa makampuni mengine nje ya hiyo familia?
Endelea kujazia nyama mkuu
 
Haijakaa sawa kukagulia gari hapa wakati imeisha ingia. Hata ikisemwa itengenezwe ni kuongeza magumashi na madili. Labda waue hiyo monopoly ya kukagulia JP, watu wawe na choices nyingi.
 
Katika hali inayoashiria mtandao wa fedha haramu, familia moja yenye uhusiano wa karibu na vigogo nchini Tanzania inadaiwa kuteka mfumo mzima wa uagizaji wa magari ya mtumba kutoka Japan, na kuelekeza mabilioni ya fedha za Serikali katika mifuko yao, huku kukiwa na mgongano mkubwa wa kimaslahi.

Katikati ya mtandao huu yupo mfanyabiashara anayejulikana kwa jina la Prosper Sugai, au Japheth Benedict Nguku. Mtanzania aliyepata uraia wa Japani, na mmiliki wa kampuni ya ukaguzi wa magari iitwayo EAA Company Limited.

Kampuni hii inatajwa kuwa kitovu cha mtandao unaodhibiti kila hatua ya safari ya gari kutoka mnada wa Japani hadi barabarani Tanzania, huku ikihakikisha hakuna mkaguzi huru anayeweza kubaini dosari muhimu.

Mtandao wa Familia

Uchunguzi umebaini muundo ulio wazi, ambapo Mkaguzi yaani kampuni ya EAA Company Ltd (ya Prosper Sugai) ndiye wakala rasmi wa ukaguzi wa magari yanayopelekwa Tanzania (Pre-Shipment Verification of Conformity- PVOC) nchini Japan.

Waagizaji ni pamoja na kampuni mbalimbali zinazomilikiwa na familia yake wa karibu, akiwamo Rosper International (mpwa Thomas Brown), Real Motors International (kaka Josiah Nguku), Yune International (kaka Yune Nguku) na Be Forward Tanzania, inayohusishwa na mpwa Daniel Mtaalam.

Katika usafirishaji, ipo kampuni ya Prime Consolidators (kaka Kevin Nguku) kwa ajili ya upakiaji, Afritel (kaka Josiah Nguku) kwa ushughikiaji wa mizigo na upitishaji forodha Tanzania.

Upitishaji wa Fedha: ipo kampuni ya Omros, yenye utata inayoendeshwa na mshirika wa karibu wa Sugai. Vyanzo vinaeleza kuwa Omros ndicho kituo kikuu cha utoaji rushwa, chenye mitandao Yokohama (Japani), Afrika Kusini, maeneo ya Caribbean, na muhimu zaidi—Miami, Marekani. Mtandao huu hufanikisha usafirishaji na kuficha faida za mtandao huu wa kifisadi duniani kote.

Mtandao huo unajenga pisha ya mgongano wa kimasilahi kwamba, inawezekanaje EAA kuikagua kwa uadilifu mizigo ya magari inayotumwa na kampuni za ndugu zao ambao wanapata faida tu kama magari yatapita ukaguzi?

Kimsingi mumo huo umetengenezwa kwa ajili ya kupitisha magari kwa muhuri wa kirafiki, bila kuzingatia ubora.

View attachment 3513874
Rais Magufuli alishtukia mchezo

Machi 2021, hayati Rais John Magufuli, kwa misingi ya utaifa, alifuta mfumo wa PVOC ambao asilimia 70 ya ada zilikwenda kwa mawakala wa kigeni kama EAA. Akaanzisha Destination Inspection (DI), ambapo TBS wangefanya ukaguzi bandari ya Dar es Salaam.

Matokeo yalikuwa ya haraka na ya kuvutia: ndani ya miezi sita, TBS ilikusanya Sh bilioni 3.9, fedha ambazo hapo awali zingewafaidisha mawakala binafsi. Serikali ilikuwa imerejesha haki yake.

Ni wazi kwamba sera ya DI ilikuwa tishio la uhai wa biashara za kina Prosper Sugai na EAA, kwani iliifuta kabisa biashara yao ya mabilioni ndani ya siku moja.

Baada ya Magufuli kufariki, mrithi wake, Rais Samia Suluhu Hassan, alitoa maagizo kwamba magari yakaguliwe kule yanapotoka akidai kuwa utaratibu wa kuyakagua yanapofika nchini una urasimu.

View attachment 3513875

Inadaiwa kuwa mpaka agizohilo linatoka, kulikuwa na ushawishi wa kampuni za ukaguzi wa magari zikitumia vigogo wa Serikali.

Inadaiwa kuwa Balozi Hussein Kattanga, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Japani (2020–2021), alihusishwa.

Taarifa Zaidi zinaeleza kuwa hatua muhimu zaidi ilikuwa kumhusisha Abdul Halim Hafidh, mtoto wa mtu mashuhuri sana ndani ya Familia ya Rais. Hafidh alifungua ofisi kamili Yokohama, Japan, na kuwa kitovu muhimu cha mtandao huu.

Kwa ushirikiano huu wenye nguvu, mabadiliko yalikuwa ya haraka.
Machi 2022, serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ilirejesha mfumo wa PVOC, kwa madai kuwa Tanzania “haina ujuzi wa kutosha,” kinyume kabisa na rekodi ya mafanikio makubwa ya TBS miezi michache tu kabla.

Vyanzo vinaeleza kuwa EAA hutenga USD 50 kwa kila gari kama malipo ya kufanikisha mfumo haramu wa mwamala. Kwa Tanzania kuagiza takribani magari 70,000 kila mwaka, hii ni USD milioni 3.5 (zaidi ya Sh bilioni 8.5) kila mwaka. Kwa mkataba wa miaka minne, mtiririko wa fedha unaofujwa unakaribia Sh bilioni 34.

Baada ya kufanikisha dili hilo, inadaiwa kuwa Balozi Kattanga, alirudishwa Tanzania na kuteuliwa Katibu Mkuu Kiongozi. Mwaka 2023 akawa Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Washington D.C na kisha mwaka 2025, EAA ikafungua ofisi mpya ya ukaguzi Miami, Marekani, ishara kuwa mtandao unazidi kupanuka kimataifa.

Madhara yake

Familia ya Sugai-Nguku, kupitia kampuni zao zilizounganishwa, inadhibiti, Kiwango cha ubora (kupitia mamlaka ya ukaguzi ya EAA), uagizaji (kupitia kampuni zao nyingi za kuagiza magari) na usafirishaji na Forodha (kupitia kampuni za ndugu zao).

Matokeo yake ni upotrevu wa fedha za Serikali, ushindani wa kibiashara umedhoofishwa na wananchi wanaishia kununua magari yasiyokaguliwa kwa usalama bali kwa faida ya mtandao huu.

Wanaoathirika ni hao wanaoagiza kwao, Mimi nikiagiza direct naathirika vipi? Hii nchi ina Matatizo mengi sana, kama ni list ya magonjwa, hii ni kikohozi tu, let's deal na mambo Makubwa!
 
Back
Top Bottom