Mtandao wa tigo - halichachi

Yaah haipo.
Ilikuwa nzuri sana, walianza tu niliweka elfu tano nikawa na dakika kama 100 za mitandao yote, sasa leo zimeisha nimetaka kurudia kumbe kuna mabadiliko, tigo bwana!!!
 
sasa hii jaza ujazwe naipata kwenye menu au?
maana hapa naona
OFA MAALUM
MIniKabang
tigo - tigo Xtreme
vifurushi vya kimataifa
internet vifurushi
University offer pia wameiondoa... Hawa jamaa washafulia ngoja nikanunue line yangu ya Halotel... Niendelee kuburidika na bando
 
Wapendwa naomba mnijuze, hivi mtandao wa tigo wamefuta ile huduma yao ya "halichachi"?

NImejaribu kubonyeza nyota 148 nyota 00 reli ili nipate hiyo option lakini siioni!!!!

dial *148*02# utakuta kifurushi kipo mimi nimejiunga muda sio mrefu
 
University offer pia wameiondoa... Hawa jamaa washafulia ngoja nikanunue line yangu ya Halotel... Niendelee kuburidika na bando
Labda hilo la vyuo vikuu watakuwa wameliondoa huu mwezi wa Ramadhan kwa kuwa kuna watu amefunga, sio mwanafunzi lakini anakwenda kuunga bando la chuo kwa hiyo anapata dhambi kwa hiyo watakuwa wamelisitisha ili wasiwatie watu waliofunga majaribuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…