masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,207
- 13,839
Katika sakata la kuonekana kuwa suala la mabomu ya Arusha ndio kwanza linaaza, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, amesema uchunguzi wa milipuko hiyo(Olasiti na Soweto) unaendelea na hakuna atakayebainika atakayeachwa atambe.
Kwa wale wenzangu na miye ambao hamsomi gazeti la Uhuru, leo wametoa freshi.
Kulingana na gazeti hilo Uhuru la Julai 4, 2013, nanukuu:
"Na Lilian Mollel,Arusha
Mtandao wa ulipuaji wa mabomu katika jiji la Arusha umebainika na kwamba, mipango yote ilianzia jijini humo, pamoja na wahusika wake.
Taarifa za awali kutoka jeshi la polisi zinasema milipuko iliyotokea katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi,Olasiti na ule wa Uwanja wa Soweto, licha ya mabomu hayo ktengenezwa nchi tofauti.
Bomu liliolipuliwa uwanja wa Soweto Juni 15 limetengenezwa nchini China na lile la Kanisani lililolipuliwa Mei 5 , mwaka huu limebainika kutengenezwa Russia na halikuwa na namba za usajili..
Imeelezwa kuwa wataalamu toka China wapo jijini Arusha wakifanya uchunguzi wa kina kuhusu bomu hilo........"
Vile vile ......
Mkuu wa Mkoa wa Arusha , Magesa Mulongo, amesema
" Alisema makachero wa polisi na vyombo vingine vya ulinzi bado wapo jijini hapa wakiendelea na kazi na kwamba mtandao huo wa walipuaji umebainika."
Wana JF msemo kuwa serikali ian mkono mrefu sasa utatimia, maana pale Arusha kuna FBI, Wachina na hata vyombo vyetu vya dola.
Hapo ndio patamu maana ukweli lazima utabainika.
Wale wenye DVR zao kama zilivyokuwa zikitamba kuwa ni polisi walihusika ni bora wakashirikiana na kuyaweka hadharani sasa ili watuhumiwa wapelekwe kwa pilato.