MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,266
Ni kweli Watanzania hawahitaji polojo na UWONGO ambapo UWONGO wako pia ulichukua muda mrefu kugundulika kwa sababu ya kutumia jina linalofanana na jina la Mwl. Nyerere huku ukijinasibisha kama wewe ni MTOTO wa Mwl. Nyerere wakati huna mahusiano yoyote yale kifamilia au kindugu na Mwl. Nyerere achilia mbali kuwa MTOTO wa Mwl. Nyerere.Watanzania hawahitaji porojo, wanahitaji kuambiwa ukweli kuwa fulani na fulani ndio waliolipua mabomu,
Bahati mbaya kwenu nikuwa hamuwezi kuwadanganya kwakuwa Wanaarusha waliona kwamacho yao mlipuaji na wapigaji risasi kuwa ni POLISI wa Tanzania,
Huwezi kuwadanganya wakati wameona na wamepigwa risasi kisa wameona, huwezi kuwadanganya kwakuwa wameona ndugu zao wakiuliwa live,
Ukitaka kudanganya nenda kaidanganye familia yako lakini naamini nayo itakukataa tu!
Kama ulijua Watanzania hawapendi UWONGO, kwa nini uliendelea kuwadanganya kwa MUDA MREFU?. Bandiko lako hili limebeba sura zote za mtu ambaye ni HYPOCRITE.
Mtoto wa Mwl. Nyerere anayeenda kwa jina la Andrew Nyerere alipouvalia njuga UWONGO wako ukajikuta huna jinsi nyingine ya kuendelea kuudanganya UMMA wa JF kama wewe ni mtoto wa Mwl. Nyerere na ukaja na STATEMENT baada ya Andrew Nyerere kuanza uchunguzi,
Nipo Butiama sasa hivi. Naulizia kuhusu huyu Yericko,lakini bado sijampata mtu anayemfahamu. Bado naendelea kuulizia. Nimemtuma mtu afanye uchunguzi.
Nilikuwa naongea na Joseph Butiku sasa hivi,na Mama Maria. Nimewauliza kuhusu huyu Yericko Nyerere. Hawamfahamu. Butiku amesema,watu wanajipa majina wanavyopenda; Adam Marwa ana mtoto wake mmoja tu,anaitwa Lumumba. Mimi[Butiku],mtoto wangu anaitwa Kaunda. Magige Nyerere ana mtoto anaitwa Moringe. Halafu Mama Maria akasema,Rose Nyerere ana mtoto anaitwa Luis Rwagasore,Mfalem wa Rwanda.
Kwa hiyo Butiku amesema huyu kijana kama angekuwa na namba ya simu,ningeweza kumtafuta,ili aweze kujieleza. Kwa hiyo nimempa Butiku namba ya simu ya Yericko Nyerere.
Watoto wengi wa Mwl. Nyerere hata sura kidogo wanafanana na baba yao, hii ya kwako hata hukuona aibu kama watu wangeilinganisha na sura ya Mwl. Nyerere.Niwashukuru sana uongozi wa JF hasa Mods kwa kuusimamia mjadala huu kwa weledi wa hali ya juu sana! Hii ni heshima kubwa sana kwa JF na Tanzania kwa ujumla!
Mwisho,
Wale mliotaka kunifahamu mimii ni nani hasa? Ninawajibu rasmi!
Naitwa: Yericko Yohanesy Nyerere
Mahali nilipozaliwa: Nyololo, Mufindi, Iringa.
Kabila: Ni Mhehe,
Baba yangu: Yohanes Msambila Nyerere, (marehemu)
Mama yangu: Venancia Geremias Mgimwa,
Elimu: Muhandisi wa Umeme na Compyuta kutoka Chuo cha Beijing Information Technology College China (BITC)
Kazi: Mfanyabiahara, Mwenyekiti Mtendaji wa Umoja wa Makampuni ya YECCO GROUP LTD yanayojishughulisha na Ujenzi wa Majengo, Ujenzi wa Mabarabara, Umeme, Teknohama, Uwakala wa Usafirishaji, Uwekezaji katika Majengo, na Usanifu na Ukadiriaji Majenzi
Kuishi: Kigamboni Mbutu,
Nina mke mmoja na watoto wa wili ambao ni Che-Lee na Su-Yang
NB:
Mimi sina UNDUGU na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, lakini chimbuko la Babu yake na Babu yangu Mzee Msambila Kihulo Lihangawike Nyerere "inasemekana" alikuwa ni wa kaskazini mwa Tanzania!
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-tanganyika-na-zanzibar-224.html#post6630081