Mtandao wa Vodacom wajitafakari

Mtandao wa Vodacom wajitafakari

Kapumpuli

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2018
Posts
2,040
Reaction score
2,674
Kwa siku za hivi karibuni mtandao wa Vodacom umekuwa ukisumbua sana Hali ambayo imepelekea usumbufu mkubwa sana kwa watumiaji wa mtandao huu.

Kumekuwa na Hali ya kukatika kwa network au kushindwa kufanya miamala ya kifedha jambo ambalo limekuwa likijirudia rudia na kuzua sintofahamu Kubwa kwa watumiaji.

Ikumbukwe kuwa mtandao huu umekuwepo nchini kwa miongo miwili Sasa na hivyo kujizolea watumiaji lukuki...

Lakini changamoto hii iliyoanza kujitokeza itasababisha watumiaji kuanza kuwakimbia...

Nitoe Rai kwa Menejimenti ya Vodacom na timu Yao ya Ufundi wajitafakari sana.

Wachukue hatua muhimu ili kuondoa changamoto hii kwa mtandao huu pendwa ambao umetumika kwa muda mrefu nchini Sasa.
 
Ukiwa na Akili timamu huwezi kuutumia huu / huo Mtandao badala yake utautumia Mtandao mzuri, wenye uhakika 100% na ambao Watu wengi wenye Akili Kubwa na Ushawishi Uliotukuka tunautumia huko Tanzania na hata hapa nchini Uganda nilipo wa Airtel.

Nikiona Mtu yoyote hatumii Mtandao wa Airtel huwa namdharau mno na wala huwa sitaki pia kupoteza muda wangu Kuzungumza nae kwakuwa najua hata Vichwani mwao pia huwa ni Watupu. Na pia Mtandao wa Airtel ni Mtandao ambao ukiutumia tu haaka sana kama ulikuwa Masikini basi Maisha yanabadilika na unakuwa Tajiri.

Imeisha hiyo.....!!
 
Ukiwa na Akili timamu huwezi kuutumia huu / huo Mtandao badala yake utautumia Mtandao mzuri, wenye uhakika 100% na ambao Watu wengi wenye Akili Kubwa na Ushawishi Uliotukuka tunautumia huko Tanzania na hata hapa nchini Uganda nilipo wa Airtel.

Nikiona Mtu yoyote hatumii Mtandao wa Airtel huwa namdharau mno na wala huwa sitaki pia kupoteza muda wangu Kuzungumza nae kwakuwa najua hata Vichwani mwao pia huwa ni Watupu.

Imeisha hiyo.....!!
Huu ni uchokozi umefanya. Lol

Ova
 
Jana ilisumbua mara mbili. Kuna muda nilikuwa na shida kweli kuna fursa niliiona ulaya huko hadi nikakwama.
 
nafikiri ipo shida mahali, kama voda inasumbua basi kuanzia leo sitaamini mtandao wowote ule!
 
Kutwa kuomba radhi kwa tatizo linalojirudia rudia

Mpendwa Mteja, Tunaomba radhi kwa changamoto uliyoipata ya miamala ya M-Pesa kwenda mitandao mingine na benki. Kwa sasa huduma zimerejea kikamilifu. Miamala ambayo haijakamilika, itakamilishwa au kurudishwa haraka iwezekanavyo. Tunakushukuru kwa uvumilivu wako.
 
Hawa wapuuzi wamenilaza giza na vyakula kwenye frdge sidhani kama vipo salama
Itanilazimu kuhamisha fedha ya umeme kwenye mitandao mingine
 
Kuna fundi anaerekebisha signal za mitandao inayosumbua sumbua anaitwa fundi kiiisamba nadhani inafaa vodacom waonane nae
 
Kesho Nahamisha vitu vyangu nusu na kuweka Tigo,Bora nipate hasara ya kutuma kuliko fedhea niliyopata leo.
Una hela hazitoki.

Bila kuwa na mtu alieniamini ningeaibika sana.
Yaani..... Imekuwa Kero kwelikweli.... Nilipita mitaa ya mwenge jirani na uwanja wa KMC.... Nimekutana na watumiaji kadhaa wakilalama baada ya miamala Yao kukwama..... Hii inasikitisha sana
 
Back
Top Bottom