Mtandao wa Vodacom wameniibia hela yangu msaada tafadhali

Mtandao wa Vodacom wameniibia hela yangu msaada tafadhali

Nagweretu

Member
Joined
Jan 21, 2020
Posts
78
Reaction score
77
Mimi ni wakala wa voda na mitandao mingine pia kwa kutuma na kutoa hela

Leo nipo ofisini kuangalia kamisheni yangu nikakuta zaidi ya 50 elfu imekatwa

Moja kwa moja nikawasiliana na huduma kwa wateja kitengo cha mawakala nikawaambia mbona mmepunguza kamisheni yangu. Wakaniambia wasiliana na kiongozi wako wa kanda (Tdr)

Tdr kuwasiliana naye ananiambia umekuwa unafanya miamala ya kutuma (kutoa)pesa kwa wakala mkuu, lakini miamala ya wakala mkuu kukutumia wewe pesa kweny code yako ya wakala ni michache

Na mimi huwa nafanya miamala ya kutoa hela kwa wakala mkuu ili anitumie kwenye mitandao mingine (Froat exchange).

Sasa nikajiuliza mbona huu kawa wizi vile kwani hakuna sms au notification niliyopewa kuwa salio lako limepunguzwa kwa sababu ya kosa fulani na hakuna elimu yoyote niliyowahi pokea kutoka VODACOM kwenye suala hilo Mitandao mingine haijawahii kunianyia kitu ya aina hii

Wale wenye uzoefu wa mambo haya naweza kufanyaje kupata msaada wa kurudishiwa hela yangu.

Au kwa upande wa sheria za mitandao suala hili likoje?
 
Natamani hata niwashitaki hawa wezi
Ila sijui nianzie wapi
Mwenye ile link ya TCRA malalamiko mtandaoni naiombeni?
 
Back
Top Bottom