Unfortunately sikuweza kuona attachment yako; ninatumia Cable 200mbs/20mbs hivyo sina tatizo la kudownload, hivyo nina imani kuwa mtandao wangu ni mzuri. Jaribu kuweka attachament yako mtandaoni vizuri tena ili tuweze kuisoma au kuiskiliza sawasawa.
Bwana Said Mohammed, lazima nianze kwa kukupongeza kuwa huwa unafanya utafiti wa historia kwa muda mrefu na kwa uhakika sana; una information nyingi sana za kihistoria kuhusu Tanzania na hilo halina ubishi. Sitakuwa mwungwana kama nitapinga ukweli huo. Tatizo lako kubwa ni kuwa huwa unaripoti matokeo ya utafiti wako ukiwa skewed kidini kuonyesha kuwa dini unayoamini ilifanya kazi kubwa sana kuleta Uhuru wa Tanganyika kuliko dini usizoamini na unadhani kuwa dini unayoamaini haipewi credit inayostahili. Imekuwa ni kawaida vitabu vyako kuuzwa kwa wingi misikitini kuliko sehemu nyingine yoyote ile kwa sababu hata mimi nimepata vitabu vyako kutokea miskitini.
Inawezekena nimetumia neno propaganda vibaya kidogo kwa vile lina maana pana zaidi ya nilivyotaka kusema. Nimeshaoma vitabu vyako kadhaa na kutambua kuwa ingawa huwa vinasema ukweli, huwa pia vinafisha ukweli mwingine kwa makusudi, jambo ambalo wenzetu wanasema TRUE BUT MISLEADING. Vitabu vyako nilivyosoma ni vya aina hiyo ambapo unaweza kuandika kuhusu Meru lakini lengo lako ni kutaka kusema kuwa Abdul alifanya mambo makubwa kuliko Nyerere lakini hatamabuliwi. Ni kweli but misleading. Sijui neno la kiswahili linalokaribiana na hali hiyo ndiyo maana nikatumia propaganda. Watu walioshiriki kugombea Uhuru wa Tanganyika ni wengi sana kuliko unavyoamini, na wala hakujawa na juhudi za serikali kimakusudi kudharau mchango wao kwa ajili ya kumtukuza Nyerere, hata hivyo ni jambo la kawaida kabisa kwa credit kwenda kwa yule aliyewaongoza ambaye ni Nyerere.
Mimi ni mwana sayansi asili (Natural Sciences) lakini ni mpenzi sana wa historia, ambaye ndiye niliyeanzisha juhudi za kutaka hili jukwaa la historia kufunguliwa hapa JF. Ninasoma sana historia kutoka kwa waandishi mbalimbali ikiwa ni pamoja na uandishi wako. Kwako nimekuwa kila mara nachambua pumba na mchele kwani huwa unazichanganya sana hasa ukizingania kuwa zote zinatokana na mpunga!
Kichuguu,
Ahsante.
Kama kuna uwezekano wa kunifahamisha attach. ambazo umeshindwa
kuzifungua tafadhali niwekee nijaribu kuziweka upya.
Hayo uliyosema kuhusu utafiti na uandishi wangu wala hukukosea kwani nia yangu
ilikuwa kuandika maisha ya
Abdul Sykes na mchango wa Waislam si tu kwa kupigania
uhuru wa Tanganyika bali hata katika kumtia
Nyerere katika siasa za Dar es Salaam ya
1950s.
Ikiwa ukweli huu huutaki mimi sina tatizo mimi nilichofanya ni kuirejesha historia ya kweli
ya TANU na uhuru wa Tanganyika kama nilivyohadithiwa na wazee wangu.
Simlazimishi mtu kuikubali niliyoandika.
Msomaji ana uhuru wa kuanza historia ya TANU na Nyerere 1952 na hata asiwataje
Abdul
na
Ally Sykes wala
Sheikh Hassan bin Amir,
Mshume Kiyate wala
Hamza Mwapachu
kwa kuwataja wachache.
Kuna tofauti moja kubwa na muhimu baina yetu.
Mimi nina taarifa ambazo wewe huna kuhusu nini kilitokea hata ikawa jina la
Abdul
Sykes na wazalendo wengine kufutwa katika historia ya TANU.
Najua pia nini kilikuwa kinehofiwa.
Na haya si kwa historia ya TANU.
Ukenda katika historia ya Vita Vya Maji Maji mambo ni hayo hayo.
Jina la
Sultani Abdul Rauf bin Songea Mbano kukupa mfano mmoja tu, limefutwa
badala yake limwekwa la
Songea Mbano na waliofanya haya wanajulikana.
Naamini wewe unajua athari ya kisaikolojia kama majina ya kweli ya wale majemadari
66 wa Maji Maji walionyongwa na Wajerumani kwenye kaburi lao la pamoja yangeandikwa
majina ya akina
Sultani Hassan bin Khamis Massaninga na wenzake.
Nadhani unajua maswali ambayo mtu angejiuliza kila akisoma jina anaingia ''bin fulani...''
Sultani Abdul Rauf bin Songea Mbano, Sultani Hassan bin Khamis Massaninga..
na huo ndiyo ukawa mtiririko...bin wa bin, bin wa bin.
Historia ya TANU nayo ni hivyo hivyo
.
Mimi sina taarifa kama kitabu changu kinauzwa misikitini ila ninachoweza kusema ni kuwa
nimeshuhudia kitabu changu kikiuzwa nje ya msikiti wa Ngazija pamoja na kitabu cha
John
Sivalon wala sikuhisi vibaya kwani mimi binafsi nimenunua vitabu kadhaa pale Cathedral
Bookshop ingawa sipaiti pale kanisani ingawa duka lile ni la Kanisa Katoliki likiwa ndani ya
uwanja wa kanisa.