Mtanganyika wa kwanza kuhutubia UN

Mtanganyika wa kwanza kuhutubia UN

kuna mmeru mmoja kama sikosei alienda kuomba Uhuru wa meru land umoja wa mataifa wakasema hawaitambui hiyo nchi wanaijua tanganyika
 
Ni justin kirilo wa meru alienda kudai ardhi walizopora masetla wa kizungu
 
Unfortunately sikuweza kuona attachment yako; ninatumia Cable 200mbs/20mbs hivyo sina tatizo la kudownload na nina imani kuwa mtandao wangu ni mzuri. Jaribu kuweka attachment yako mtandaoni vizuri tena ili niweze kuisoma au kuisikiliza sawasawa.

Bwana Said Mohammed, lazima nianze kwa kukupongeza kuwa huwa unafanya utafiti wa historia kwa muda mrefu na kwa uhakika sana; una information nyingi sana za kihistoria kuhusu Tanzania na hilo halina ubishi. Sitakuwa mwungwana kama nitapinga ukweli huo. Tatizo lako kubwa ni kuwa huwa unaripoti matokeo ya utafiti wako ukiwa skewed kidini kuonyesha kuwa dini unayoamini ilifanya kazi kubwa sana kuleta Uhuru wa Tanganyika kuliko dini usizoamini na unadhani kuwa dini unayoamaini haipewi credit inayostahili. Imekuwa ni kawaida vitabu vyako kuuzwa kwa wingi misikitini kuliko sehemu nyingine yoyote ile kwa sababu hata mimi nimepata vitabu vyako kutokea miskitini.

Inawezekena nimetumia neno propaganda vibaya kidogo kwa vile lina maana pana zaidi ya nilivyotaka kusema. Nimeshaoma vitabu vyako kadhaa na kutambua kuwa ingawa huwa vinasema ukweli, huwa pia vinafisha ukweli mwingine kwa makusudi, jambo ambalo wenzetu wanasema TRUE BUT MISLEADING. Vitabu vyako nilivyosoma ni vya aina hiyo ambapo unaweza kuandika kuhusu Meru lakini lengo lako ni kutaka kusema kuwa Abdul alifanya mambo makubwa kuliko Nyerere lakini hatamabuliwi. Ni kweli but misleading. Sijui neno la kiswahili linalokaribiana na hali hiyo ndiyo maana nikatumia propaganda. Watu walioshiriki kugombea Uhuru wa Tanganyika ni wengi sana kuliko unavyoamini, na wala hakujawa na juhudi za serikali kimakusudi kudharau mchango wao kwa ajili ya kumtukuza Nyerere, hata hivyo ni jambo la kawaida kabisa kwa credit kwenda kwa yule aliyewaongoza ambaye ni Nyerere.

Mimi ni mwana sayansi asili (Natural Sciences) lakini ni mpenzi sana wa historia, ambaye ndiye niliyeanzisha juhudi za kutaka hili jukwaa la historia kufunguliwa hapa JF. Ninasoma sana historia kutoka kwa waandishi mbalimbali ikiwa ni pamoja na uandishi wako. Kwako nimekuwa kila mara nachambua pumba na mchele kwani huwa unazichanganya sana hasa ukizingania kuwa zote zinatokana na mpunga!
Utajichosha bure, huwa hasikii.
 
Marytina tuheshimiane, mimi sifanyi siasa bali nafanya utafiti. Na huwezi kupingana na historia. Utapata wapi siasa leo usipoanzia jana. Ignorance of history made man to repeat same mistakes.
Sasa huo utafiti wako mkuu ndio utwambie nani alihutubia UN kama mtanzania wa kwanza juu ya nini povu?
 
Back
Top Bottom