Nianze kwa kusema nina mashaka na Uzi huu kuondolewa kwani kuna hisia kuwa kwa sasa Mhariri (mod) wa jukwaa la siasa JF anafanyia Nazi zake Lumumba. Hivyo chochote wasichokipenda wao hapo basi kitaondolewa au kwenda kuchomekwa hata jukwaa la "utabiri wa hali ya hewa"
Hoja ya msingi hapa ni kuwa Mheshimiwa Magufuli kwa sasa ni mtangaza nia na anasubiri maamuzi ya wenye chama (wanachama) wampitishe kuwa mgombea.
Hata kama kafanya alivyoweza kufanya kuhakikisha fomu za JMT inatolewa fomu moja tuu, jee mamlaka ya kuwa msemaji wa uchaguzi wa Rais wa Zanzibar hadi kutoa maonyo kayatoa wapi?
Zanzibar ni nchi na anayechaguliwa sio mkuu wa mkoa Bali Rais anayepigiwa naye mizinga kama yeye tuu kwa nini awaonye wachukua fomu kuwa ni wengi?
Kwa majibu mepesi utaambiwa anayo mamlaka kwa sababu yeye ndie mwenyekiti wa ccm taifa, na hapo ametumia mamlaka ya uenyekiti. Lakini kwa maoni yangu naona suala la zanzibar kwa ujumla bado ni nyeti mno.
Kama znz ni nchi je rais wa znz akivuka maji anakuwa na cheo gani?
Kama znz ni nchi je imeungana na nchi gani ili iwe sehemu ya jamuhuri ya muungano?
Kama znz si nchi je kwa nini iwe na rais?
Kama znz si nchi je kwa nini iwe na serikali?
Yaani kuna mambo mengi sana yakufikirisha kuhusu zanzibar.